TFF
KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya
wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na
Kocha Rogasian Kaijage.
Kocha Kaijage
aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na
vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya
marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.
Twiga Stars
ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika
mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex,
hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.
TFF tunaunga
mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa
Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni
kitu cha kwanza.
Twiga Stars
itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo
itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.
Boniface
Wambura Mgoyo
Media and
Communications Officer
Tanzania
Football Federation (TFF)
![]() |
| Mwenyekiti
TWFA/WFC Lina P. Kessy |
Grassroot
programme kusheheresha Siku ya wanawake Duniani
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania kwa kupitia kamati ya wanawake na chama cha mpira
wa miguu kwa wanawake wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.Mpira wa
miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika
na hata hapa nyumbani.Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu
imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika
kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi
zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF /TWFA
wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu
wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama
cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule 15
za mkoa wa Tanga.
Walimu hao
watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la
Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni matumaini ya
shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira
wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina
mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake
Mwenyekiti
TWFA/WFC
Lina P. Kessy

No comments:
Post a Comment