![]() |
| MKUU wa wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu |
Na
Mwandishi Wetu, Muheza
MKUU
wa wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu amesema wilaya hiyo imeanzisha
doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya misitu na ukanda wa bahari kwenye kata
za Kigombe ili kuweza kukabiliana na wimbi la uharibifu wa mazingira hususani
ukataji wa miti.
Mgalu
alitoa kauli hiyo wakati akisoma taarifa fupi ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa
wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kwa
kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
wilaya hiyo pia imewaondoa wavamizi waliovamia misitu ya Kwani na Tongwe
ikiwemo kupandwa miti ipatayo 1,500,000 ya matunda ,kuni,kivuli na viungo
iliyopandwa kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususani shule,mashirika
binafasi kwa ajili ya kuendeleza hifadhi ya mazingira.
Aidha
aliongeza kuwa kumekuwa na uharibifu wa tatizo la uharibifu wa mazingira na
ukataji miti unaochochewa na mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo,mbao kwa
ajili ya samani na maeneo ya kulishia mifugo.
| Uharibifu wa Mazingira Wilayani Muheza umepelekea kukauka kwa baadhi ya vyanzo maji na kusababisha uhaba mkubwa wa Maji katika maeneo mengi ya Wilaya hiyo sasa Wakazi wake hulazimika kufuatamaji zaidi ya kilimeta 10 ktk Mji wa Pongwe kama wanavyoonekana pichani wakiwa na madumu yao |
Alieleza
kuwa licha ya kulishia mifugo kumekuwa na uchimbaji haramu wa madini katika
msitu wa asili wa amani ambapo serikali imechukua hatua mbalimbali ili
kudhibiti tatizo hilo la uharibifu wa mazingira.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema wameanzisha kampeni dhidi ya athari za moto na kufanyika
vijiji 32 vilivyo karibu na misitu ili kunusuru bionuai ikiwemo kuhamasishwa
wananchi kufanya shughuli za ufugaji wa nyuki na upepo ambazo ni rafiki wa
mazingira pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa misitu na athari za
uharibifu wa mazingira.
Hata
hivo,Mgalu alizungumzia suala la migogoro ya ardhi kwenye wilaya hiyo alisema
mingi kati ya hiyo inahusu uvamizi wa mashamba makubwa ya mkonge ambayo
hayaendelezwi ipasavyo pamoja na mipaka ya wilaya inayohusiana na vijiji
vilivyopo mipakai ikiwemo mashamba saba ya mkonge,shamba la mifugo lililopo
Azimio na shamba la mifugo Mivumoni.
Aliongeza
kuwa mgogoro uliopo kati ya Muheza ,Tanga na wilaya ya Pangani hatua za
kuuupatia ufumbuzi unaendelea kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa na ule kati
ya wilaya ya Muheza na Pangani mazungumzo kati ya uongozi wa wilaya hizo mbili
bado yanaendelea ili kufikia muafaka.


No comments:
Post a Comment