



Sauti za ngoma za asili zilivutia hata kwa mbali, sauti za watu
wenye furaha wakiimba na kucheza kwa mbwembwe zilisikika, kwa wageni ilikuwa
rahisi kuhoji, Tanga kunani? Ni midundo ya ngoma ya kisambaa kutoka katika
ofisi za ‘Ubiri Women Group’ zinazotazamana na soko kuu la Lushoto, karibu
wageni karibu tudansi kwa pamoja, ni siku ya furaha, ni alhamisi ya Machi 6,
siku ya gulio Lushoto, siku mbili kabla ya maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani.
Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa LBITC, Eustard Rwegoshora, aliwakaribisha wageni waalikwa na kuwataka wanawake kusherehekea siku yao kwa amani, upendo na utulivu huku wakijipima ni wapi wametoka na wapi wanaelekea kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya kuchochea mabadiliko.
Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa LBITC, Eustard Rwegoshora, aliwakaribisha wageni waalikwa na kuwataka wanawake kusherehekea siku yao kwa amani, upendo na utulivu huku wakijipima ni wapi wametoka na wapi wanaelekea kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya kuchochea mabadiliko.
Akizungumza na washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani, mwigizaji JB alisema alivutiwa kujiunga na kampeni ya maswala ya
chakula kwa sababu anazitambua changamoto nyingi wanazokutana nazo wakulima
kwani hata yeye aliwahi kufanya biashara ya mahindi.
JB aliendelea kuelezea jinsi ambavyo alitoa machozi mara ya mwisho alipotembelea wakulimaLushoto ambapo alikutana na mkulima ambaye alimsimulia jinsi ambavyo alilima shamba zima la kabichi lakini hakuuza hata kidogo kwa kukosa wateja hivyo shamba zima likaharabika.
Akitoa mfano mwingine, balozi huyo wa chakula alisimulia kuwahi kukutana na wakulima ambao walimwambia wanatembea hadi umbali wa kilomita saba kwenda sokoni kuuza mazao yao na kwamba wakati mwingine hukosa wateja hivyo kuamua kuacha vyakula hapo sokoni vikiharibika badala ya kurudi navyo umbali huo huo mrefu.
JB alielezea kusikitishwa na jinsi ambavyo vijana wamekimbia sekta ya kilimo na kuwaacha wanawake na wazee kwa kudhani kilimo hakilipi.
Balozi huyo wa kampeni ya Grow alitumia fursa hiyo pia kupongeza shirika la Oxfam kwa kuonyesha njia kwa kuweka kontena la kuhifadhia chakula ‘cold room’ Lushoto. JB pia aliipongeza serikali ambayo kupitia wizara ya kilimo imeongeza kontena moja jingine hivyo kuyafanya kuwa mawili na hata kwenda mbali zaidi kwa kujenga jengo la kuchambulia mazao na kuyapanga kwa makundi ya ubora.
Makontena hayo hutumika kuhifadhi mboga mboga na matunda kwa kipindi kirefu hivyo kuzuia bidhaa hizo kuharibika.
No comments:
Post a Comment