CHELSEA KUTENGA ZAIDI YA EURO MILIONI 36 KWA AJILI YA DIEGO
COSTA.

KLABU ya Chelsea
imeanza mikakati ya kumnasa mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa
katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Vinara hao wa Ligi Kuu wako
tayari kutoa zaidi ya euro milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji
huyo. Tayari wawakilishi wa Chelsea wameshaomba kukutana na kambi ya Costa
na mazungumzo zaidi yanatarajiw akufanyika wiki ijayo. Chelsea wamepania
kumnasa nyota huyo kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi na kuanza kwa michuano
ya Kombe la Dunia ambayo anatarajiwa kuiwakilisha Hispania kutetea taji
lao. Costa mwenye umri wa miaka 25 tayari amefunga mabao 31 katika mechi
41 alizocheza msimu huu katika mashindano yote huku akimfuatia Ronaldo mwenye
mabao 26 kwa ufungaji wa mabao kwenye La Liga akiwa na mabao 23.

MENEJA
wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amedai kufanya machache kuwageuza
nyota wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta kuwa wachezaji bora
duniani. Viungo hao wa kimataifa wa Hispania wakiwa chini ya Guardiola
alipokuwa Camp Nou waliiwezesha timu hiyo kunyakuwa mataji 14 kutoka mwaka 2008
mpaka 2011, yakiwemo mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Xavi
na Iniesta pia walikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Hispania kilichonyakuwa
mataji ya Ulaya sambamba Kombe la Dunia, na Guardiola amedai kuwa wachezaji wa
aina hiyo hawahitaji kocha ili wacheze katika kiwango bora. Guardiola
amesema wachezaji wa Barcelona wanajipa msukumo wenyewe, hajawahi kuwafundisha
Xavi na Iniesta kucheza soka kazi yake ilikuwa ni kutoa msaada wa kiufundi
kwani wamekuwa wakicheza vyema kwa miaka 20.
MASHABIKI
wa klabu ya Manchester United wamemgeukia kocha wa zamani wa timu hiyo Sir Alex
Ferguson baada ya kuona wakipokea kipigo kutoka mahasimu wao Manchester City
katika Uwanja wa Old Trafford jana usiku. City ambao waliwasambaratisha
majirani zao hao kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Edin Dzeko na Yaya Toure,
waliamsha hasira kwa mashabiki hao na kuanza kuonyesha mabango ya kumlaumu
Ferguson ambaye ndiye aliyemchagua David Moyes kuchukua nafasi yake. Mbali
na kumshambulia Ferguson lakini pia kulikuwa mabango mbalimbali ya kumpinga
Moyes kwenye mchezo huo. Hasira za mashabiki hao zimeibuka kutokana na
timu hiyo kushindwa kufanya vyema msimu huu hususani katika uwanja wao wa
nyumbani.
No comments:
Post a Comment