![]() |
| LANGO LA MAKTABA YA JIJINI TANGA |
| JENGO LA MAKTABA JIJINI TANGA |
Wakazi wa mkoa
wa TANGA wanashauriwa kusoma vitabu, majarida
na kumbukumbu za kihistoria
vinavyo patikana katika maktaba
kuu iliopo mkoani hapa.
Amebainisha hayo mkutubi mkuu MARTINE CHAMBO wakati
akizungumza na mwandishi wa kituo hiki amsema kuwa kila mkazi anaruhusiwa
kujisomea katika mataba hiyo kwani ipo kwaajili ya kila mmoja wetu lengo la
maktaba hiyo ni kufanya jamii wakiwemo watoto vijana na watu wazima kuwa na moyo wa kujisomea.
Hata hivyo
CHAMBO amsema wanatumia mbinu
mbalimbali za kuhamasisha watu kusoma
kwa kutumia elimu kwa njia ya michezo na
burudani ilikuwavuta watu kwenye maktaba
hiyo.
Pia akusita
kutoa wito kwa jamii kujitokeza kwa
wingi katika maadhimisho ya miaka hamsini
tangu kuanzishwa kwa maktaba hiyo yakatakayo fanyika tarehe 25/03 hadi
tarehe 1/04 ambayo yataambatana na maonyesho na burudani katika maktaba hiyo.

No comments:
Post a Comment