![]() |
Kombora aina ya Sayyad-2 lililotengenezwa na wataalamu
Wairani
|
Waziri wa Ulinzi Iran Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema Iran inaweza kutengeneza makombora ya kila aina.
Akizungumza Jumamosi, Dehqan amesema, 'leo tunaweza kutengeneza aina mbali mbali za makombora yakiwemo ya ardhi kwa ardhi, ardhi kwa anga na anga kwa ardhi'.
Amendelea kusema kuwa umbali, ustadi na uwezo wa makombora ni nukta muhimu kwa sekta ya ulinzi Iran na kuongeza kuwa, Iran imefanikiwa kutengeneza makombora yenye kukwepa rada.
Aidha Brigedia Jenerali Dehqan amesema Iran sasa inamiliki teknolojia ya hali ya juu sana katika sekta ya ulinzi na hivyo ina uwezo wa kukabiliana vilivyo na vitisho vya maadui. Afisa huyo wa ngazi za juu jeshini amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kuimarisha uuzaji wa zana zake za kivita katika uga wa kimataifa.
Katika miaka ya hivi karibuni Iran imefanikiwa kuimarisha uwezo wake wa kujihami kwa kujitengenezea zana zote muhimu za kivita. Hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu inajitegenezea ndege za kivita, nyambizi, meli za kivita, vifaru n.k. Iran imesisitiza mara kwa mara kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine kwani sera zake za ulinzi zimejengeka

No comments:
Post a Comment