![]() |
|
RPC
MUNGI
|
Na Diana Bisangao wa
matukiodaima.com Iringa
..................................................................................
WATU watatu wafariki dunia
mkoani Iringa katika matukio manne tofauti likiwemo la mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Zawadi Mlaso(35) mkazi wa Mahenge wilaya ya Kilolo kufariki dunia
baada ya kupigwa risasi.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 2 machi majira ya
saa 3:30 usiku.
Kamanda Mungi alisema marehemu
alipigwa maeneo ya shingoni na silaha aina ya gobore linalotumia goroli hata
hivyo watu waliompiga hawajafahamika na chanzo cha tukio bado kinachunguzwa.
Katika tukio lingine mtu mmoja jina
Richard Leonard (29) mchimbaji wa madini eneo la Saadan alifariki dunia baada
ya kutumbukia kwenye shimo la madini lenye urefu wa futi 50.
Kamanda alisema tukio hilo lilitokea
mnamo tarehe 28 februari majira ya saa 2 kamili usiku katika machimbo ya madini
ya Ihazutwa wilaya ya Mufindi ambapo marehemu alifariki papo hapo baada ya
kutumbukia.
Mtu mmoja jina Thobias Mwangunguro
(32) mchimbaji wa madini maeneo ya Ulata, kata ya Kiponzero wilaya ya Iringa
Vijijini alifariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.
Kamanda alisema tukio hilo lilitokea
mnamo tarehe 28 februari majira ya saa 10 kamili alfajiri na kusema marehemu
alipata ajali ya kutumbukia kwenye shimo la madini na kupata maumivu makali.
Mbali na matukio hayo matatu ya vifo
Kamanda Mungi alisema JESHI la polisi mkoani hapa linamshikilia Fadhil Mahimba
(20) mkazi wa Gangilonga kwa kosa la kukutwa na misokoto 40 ya bangi.

No comments:
Post a Comment