![]() |
| Mh Samwel Sitta |
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maaalum la Katiba Mh Samwel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 469 dhidi ya mpinzani wake Hashim Rungwe Sponda katika Uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita huko Mjini Dodoma.
Akitumia kaulimbiu yake isemayo" kazi kwa Viwango na Kasi" Sitta aliweza kuwavutia Wajumbe wengi ambapo awali kabla ya kupatiwa nafasi ya kujieleza mbele ya Wajumbe alikuwa amekwisha sambaza nyaraka zinazoonesha wasifu na sera zake kwa wajumbe hao tofauti na Mh Rungwe ambaye alijikuta akikosa muda wa kutosha kujinadi baabada ya dakika 3 alizopewa kuisha kabla hajamaliza kutoa maelezo yake.

No comments:
Post a Comment