![]() |
| MKUU wa wilaya Handeni, Mh Muhingo Rweyemamu |
Na
Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU wa wilaya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, amesema kwamba ni aibu kubwa kwa wilaya yake kuomba chakula lich
licha ya kuzalisha chakula kingi kwa mwaka.
Akizungumza na wanahabari
wilayani hapa, Rweyemamu alisema kuwa hali hiyo inampa wakati mgumu, maana wao
ni miongoni mwa wilaya zinazoheshimika katika kuzalisha zao la mahindi.
Alisema wafanyabiashara wengi wanaingia
Handeni kununua mahindi, hivyo ni wakati wao sasa kuliangalia jambo hilo kwa
kina na kuleta tija.
“Kwanza lazima tupige vita kuuza
mahindi bila kuweka akiba yetu na familia zetu, maana huo ni mpango mbaya
unaotufanya tuombe chakula kila mwaka.
“Nikienda mjini kuomba omba chakula
napata wakati kwasababu tuna ardhi ya kutosha na wakulima wetu wengi wanalima,
ila mwisho wa siku wanauza hadi akiba za kula wao na watoto wao,” alisema
Rweyemamu.
Kwa mujibu wa Rweyemamu, wananchi wote
na wakazi wa Handeni wanapaswa walime sana, huku wakijiwekea akiba badala ya
kuuza chakula chao, hivyo kuifanya wilaya hiyo ikumbwe na njaa kila wakati.

No comments:
Post a Comment