|
Rukia Fungameza[20]mkazi
wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Anaetuhumiwa kutupa mtoto chooni
|
|
Hii ndilo shimo la choo alimotumbukizwa mtoto
huyo
|
| WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA |
| Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza mwenye Flana ya bluu akiwa na barozi kushoto na mashuhuda wengine wakimsikiliza mwenyekiti huyo |
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rukia
Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutupa chooni kichanga jinsi ya kiume na
kusababisha kifo chake.
Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza amesema walimtilia shaka
mtuhumiwa Februari 18 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji baada ya
kutoonekana na ujauzito,ndipo walipomuulza kulikoni naye kudai kuwa amejifungua
lakini mtoto yupo nyumbani.
Kauli hiyo haikumridhisha Mwenyekiti huyo ndipo alipoamua
kumtafuta balozi wake aitwae Daud Dule na kumuuliza mtoto yupo wapi ndipo
alipoanza kuwa na wasiwasi hali iliyowalazimu kumkamata kutoa taarifa kituo cha
Polisi Iyunga ambapo kabla ya kufika Kituoni majira ya saa kumi na moja jioni
mtuhumiwa alikiri kujifungua na kutupa kichanga chooni Februari 18 mwaka huu.
Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa
kituo kikuu cha kati Febuari 19 ambapo Polisi hawakuweza kufika eneo la tukio
licha ya Mwenyekiti wa mtaa kufuatilia mara kwa mara kwa mkuu wa kituo cha
Polisi Iyunga ambapo alijibiwa kuwa watafika.
Hata hivyo baada ya Polisi kutofika eneo la tukio kwa siku
mbili tangu kukamatwa mtuhumiwa Mwenyekiti wa mtaa alitoa taarifa katika kikao
cha kata Februari 21 kufuatia tukio
lililotukia mtaani kwake na Polisi kushindwa kufika kwenye tukio siku tatu
baada ya tukio hali ambayo ilikuwa kero mtaani kwake.
Polisi walifika eneo la tukio Februari 22 majira ya saa tano
na nsu asubuhi wakiambatana na Kikosi cha Zimamoto Jiji la Mbeya ndipo
walipoanza anza kuibua mwili wa mtoto ambapo ulikutwa umeharibika vibaya
kutokana na kukaa kwa muda wa siku nne bila kuibuliwa umbali wa kilometa saba
tu kutoka Jijini.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa alidai sababu za kutupa
kichanga hicho cha kiume ni kutokana na kuogopa aibu kwa mumewe aliyepo Songea
mkoani Ruvuma kikazi ambapo mimba hiyo aliipata nje ya ndoa.
Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo aliagizwa na mumewe
kurejea Songea mwishoni mwa mwaka jana lakini alikataa akidai kuwa angeenda
mwaka huu baada ya kumsaidia kaka yake shughuli za palizi.
Kabla ya kichanga kilichotupwa chooni mtuhumiwa ana mtoto
mwingine jinsi ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili na nusu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa amelilalamikia Jeshi la
Polisi kwa kutoenda eneo la tukio mapema hali ambayo inasababisha wananchi
kujichukulia sheria mkononi hali ambayo inweza kuepukika.
Baadhi ya mashuhuda akiwemo mama Emilly Amnoni na Paulo
Mbawala wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo kwani wamedai
ni cha kinyama na ni cha kwanza mtaani kwao hivyo wanaomba sheria iweze
kuchukua mkondo wake ili kukomesha kabisa vitendo vya kikatili Mkoani Mbeya.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment