| MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA |
Mkakati wa kuboresha
shule ya ufundi iliopo mkoani hapa umetamkwa rasmi na mwenyekiti wa kamati ya
uboreshaji shule hiyo Mkuu wa mkoa wa TANGA Bi Chiku Gallawa katika kikao na
waandishi wa habari ofisini kwake.
Gallawa amesema
Sekondari ya Tanga ufundi ni shule kongwe nchini yenye historia ndefu tangu
enzi za utawala wa kijerumani mwaka 1895 ikiwa katika eneo la awali mkwakwani
ambapo kwa sasa ipo shule ya old Tanga.
Kwasasa shule hiyo iko eneo la makorora,
ambako imeamishiwa na kufunguliwa rasmi na Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya
Muungano Tanzania hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias k Nyerere mnamo tar
31/1/1967.
Hata hivyo Gallawa
amesema hii ni shule ya kipekee katika historia ya elimu Tanzania kwani ni
Sekondari ya kwanza katika nchi hii na imetoa viongozi wengi ikiwa ni pamoja na
Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.
Pia amesema kutokana
na umuhimu wa shule hii wameona uko umuhimu wa kukarabati ili kuweza kurudisha
shule hii katika historia yake kuienzi na hatimaye iendeleze kutoa wataalamu na
viongozi wa ngazi mbalimbali
Shule hii ina majengo
yenye umri 47 na miundo mbinu yake ni ya zamani kwani kwa muda mrefu
haijafanyiwa ukarabati hivyo kufanya miundo mbinu kuwa katika hali mbaya
maeneo yanayo hitaji ukarabati ni madarasa,maabara,
No comments:
Post a Comment