![]() |
| Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania. |
![]() |
| Mgeni Rasmi katika kongamano la viongozi wa dini na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya akifungua kongamano ambapo viongozi hao walijadiliana na kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania. |
![]() |
| Sheikh Abubakar Zuberi akitoa mada ya Mtazamo wa Kiteolojia/Kidini juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini wakati wa kongamano la viongozi hao mjini Mtwara. |
![]() |
| Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara. |
![]() |
| Hiki ni moja ya kisima cha gesi kilichopo Mnazi Bay eneo la nchi kavu kinachofikisha idadi ya visima vitatu ambapo kimoja kipo eneo la bahari kuu. |
RASILIMALI
za gesi asilia, mafuta na madini zilizopo mikoa ya Lindi na Mtwara ni
kwa neema, ukarimu, ufadhili na baraka za Mwenyezi Mungu alizoipatia
Tanzania zitumike kwa manufaa ya wanachi wote.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mgeni rasmi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikani
Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya alipokuwa akifungua kongamano la Viongozi
wa Dini leo katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mjini Mtwara.
Kongamano
hilo la viongozi wa dini liliongozwa na kauli mbiu iliyosema
“Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo
ya Tanzania”.
Lengo
la kongamano la voingozi wa dini lilikuwa ni kupata elimu juu ya
rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kwa minajili ya haki,
upendo na amani kwa kuzingatia sera na taratibu za Serikali kwa maslahi
ya wananchi wote.
“Pamoja
na sheria na sera za rasilimali za gesi, mafuta na madini zilizopo
nchini, ni lazima ziongozwe na misingi muhimu ya taifa letu” alisema
Askofu Dkt.Chimeledya.
Dkt.
Chimeledya aliitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na haki ya kila
mtanzania, ukweli juu ya sera mipango na mikakati bora, mshikamano wa
jamii, kujali maslahi ya wote na ushirikishwaji wa jamii zilizo katika
maeneo yanayozunguka sehemu zilipo rasilimali mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi
alisema kuwa Serikali kupitia Wizara yake ipo tayari kuendelea
kushirikiana na vingozi wa dini wa wanachi wote ili kuendelea kusukuma
mbele maendeleo ya nchi kwa manufaa ya watu wake.
“Gesi
ni ukombozi ni ukombozi na itatusogeza mbele ambapo italinufaisha taifa
katika Nyanja mbalimbali, viwandani, majumbani na ndani ya nchi hata
nje ya nchi” alisema Maswi
Kugunduliwa
kwa gesi mikoa ya Lindi na Mtwara kumefungua milango ya kujengwa
viwanda mabalimbali ambavyo vinatajiwa punguza tatizo la ajira katika
mikoa hiyo na nchi nzima kwa ujumla.
Miongoni mwa viwanda vya saruji vinavyoendelea kujengwa ni Dangote kilichopo Mtwara na Meis kilichopo mkoani Lindi.
Katibu
Mkuu Maswi ametoa rai kwa watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kupitia
viwanda wafikirie kuwekeza juu ya viwanda vinavyozalisha bidhaa
zinazotumia malighafi zinazotokana na mabaki gesi baada ya kuchakatwana
ikiwemo viwanda vya mbolea, plastiki, chupa na nguo.
Viongozi
hao wa dini walipata fursa ya ziara ya kutembelea mitambo ya kusafisha
gesi na visima vya gesi Mnazi Bay eneo la Msimbati na eneo la juenzi wa
mitambo ya kusafisha na kuchakata gesi kilichopo eneo la Madimba mkoani
Mtwara.
Kongamano
kwa viongozi wa dini ni la siku mbili ambapo linawashirikisha viongozi
wa dini mbalimbali za kikristo na kiislam kutoka mikoa ya Lindi na
Mtwara pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya
Nishati na madini na mashirika yaliyo chini yake ya TANESC, TPDC NA REA.
Kongamano
hilo ni muendelezo ulitokana na kongamano kama hilo lililofanyika
Januari 2014 jijini Dar es salaam ambapo wajumbe kutoka mikoa ya Lindi
na Mtwara waliona kuna haja wao kama wadau wa gesi, mafuta na madini
wapate elimu kama hiyo kwa manufaa ya wanachi wa mikoa yao na nchi
nzima.





No comments:
Post a Comment