HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 17 February 2014

SERIKALI YAOMBWA KUTOA ENEO KWA AJILI YA MRADI WA UFUGAJI WILAYANI HANDENI


MKUU WA WILAYA YA HANDENI MHINGO RWEYEMAMU



SERIKALI imeombwa kutenga eneo lenye ukubwa wa hekta 2000  kwajili ya kuboresha mradi wa Ng'ombe wa nyama aina ya Borani na Sewali uliopo katika  kijiji cha Taula Kata ya Kwedizinga Wilaya ya  Handeni Mkoani Tanga.

Akizungumza na wanahabari,Mwenyekiti wa Kampuni ya Masaya Farm  Limited Sabas Woiso alisema kuwa matarajio yao ni kufikia hadi Ngombe 1500 wenye tija  ambao utawapelekea kuingia katika soko la ndani na nje ya nchi kwa kupitia mradi huo.

Owiso amesema hivi sasa wana eneo dogo ambalo ni hekta 120
ukilinganisha na mifugo iliyopo kuwa mingi na kila ngombe mmoja
anatakiwa kutengewa hekta moja kwa mzunguko wa mwaka tofauti na eneo walilonalo hivi sasa  ambapo  wana Ngombe 123, Ndama 21 na baadhi yao kuwa wajawazito hivyo itapelekea kuwa na msongamano mkubwa  katika eneo hilo.

Owiso amesema kuwa wafugaji wamekuwa wakifuga mifugo yao kwa mazoea  hivyo kwa kupitia mradi wao wananchi wa kijiji hicho watajifunza namna ya ufugaji bora na wenye tija kutoka katika  maeneo husika sambamba na kupanua soko la Tanzania.

Hata Hivyo Owiso amesema kulingana na mradi huo wananchi wa eneo hilo  watafaidika na gesi ya umeme utakaozalishwa  kutokana na kinyesi cha Ngombe  (Bayogesi),  sambamba na kupata  ajira, pamoja na kujifunza mbinu za ufugaji bora na wenye tija na kuachana na ufugaji wa mazoea.

 "Tukipata eneo la kutosheleza tutaongeza idadi kubwa ya wanyama  hawa na tunategemea kujenga uzio ambao utadhibiti afya ya Ngombe huyo ili asipate magonjwa toka kwa ngombe wengine  na  soko letu litakuwa ndani na nje kulingana na mahitaji husika na kama wadau tutajikita katika kusaidia  na kushiriki  shuguli za kimaendeleo za kijiji kama vile uchangiaji wa zahanati ya kijiji, Shule, maji, elimu......."alisema Owiso.

Naye Mshauri wa mradi huo Tadei William ameiomba serikali itoe elimu  kwa wafugaji wadogo wadogo ili waweze kuondokana na tabia ya ufugaji wamazoea na kujikita katika ufugaji  wa kisasa na wenye tija ili aweze kufaidika na ufugaji wake.

William amesema kuwa kupitia elimu hiyo wafugaji watajifunza mbinu za  kuachana na ufugaji wa kuhamahama ambao unaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa kutokana na mifugo yao kutembea ovyo hali kadhalika  itasaidia kuepusha wanyama wasiokuwa na mpangilio maalumu ya mifugo yao.

Mshauri huyo amesema serikali ihamasishe swala la mgao wa upimaji wa  maeneo ya wafugaji na wakulima ili kuweza kuwa na mpangilio utakaoweza kuepusha utembeji wa wanyama kiholela na isimamie kwa umakini matumizi bora ya ardhi yatakayoepusha migogoro kati ya wafugaji na wakulima inayorindima siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment