![]() |
| Mwenyekiti wa kamati Mh James Lembeli |
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasiri na Mazingira
imeitaka serikali kuondoa kodi kwenye vifaa vya mradi wa ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu unaoendeshwa na Shirika la Nyumba Tanzania
(NHC) ili kumuwezesha mwananchi wa hali ya chini kuondokana na makazi
duni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli aliyasema hayo baada ya taarifa ya mradi huo iliyosomwa mbele ya kamati hiyo na Mkurugenzi wake, Benedict Kilimba na kueleza kuwa kodi za serikali zimesababisha bei ya nyumba hizo kuwa kubwa.

| NYUMBA ZA NHC ZILIZOKO MKINGA |
Kwamujibu wa taarifa ya meneja huyo ni kwamba mfumo wa
kuwataka wanunue vifaa vya ujenzi kwenye maduka maalumu
kumeongeza gharama ya ujenzi huo na kufikia tsh mil, 31.3 kwa
nyumba yenye vyumba viwili na tsh mil, 35.3 hadi tsh mil, 36.2 kwa vyumba
vitatu bila VAT.
Kilimba alidai kuwa mbali na changamoto hizo shirika pia linalazimika kuilipa serikali kiasi cha tsh mil, 7 mpaka tsh mil, 10 kama kodi ya ongezeko la thamani VAT kutokana na manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa kila nyumba jambo lililosababisha nyumba hizo kuuzwa tsh mili, 40. 7 kwa nyumba ya vyumba viwili na tsh million 46. 3 hadi tsh mil, 48.2 kwa vyumba vitatu.
Hata hivyo alieleza kuwa kama shirika litaruhusiwa kutafuta maduka yenye unafuu na serikali ikaondoa kodi ya VAT mauzo ya nyumba hizo yangeweza kufikia tsh mili, 28 bei ambayo mtu wa hali ya chini angeweza kuimudu tofauti na ilivyo sasa
Akizungumza baada ya taarifa hiyo, Lembeli alisema ni wajibu sasa kwa serikali kuonyesha moyo wa dhati katika kuwawezesha wananchi kumudu kubadilisha maisha yao ikiwemo hili la makazi bora ambayo ni haki ya kila mtu.
Aliahidi kubeba jukumu la kuishauri serikali kuondoa kodi ya VAT kwenye vifaa vya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na mradi wa shirika hilo hasa zile zilizolengwa kwa ajili ya makazi bora kwa watu wa hali ya chini.
“Sisi wanakamati tumetembea katika nchi mbalimbali kama vile nchi ya Singopore, tumejionea na kujifunza jinsi serikali ya nchi hiyo inavyowawezesha watu wake katika makazi bora……..takriban asilimia 90 ya nyumba zilizojengwa na serikali ya nchi hiyo zimeuzwa kwa wananchi kwa bei nafuu, vipi sisi huku!” alihoji Lembeli.
Hata hivyo alidai kuwa taarifa ya shirika hilo kuhusu mazingira ya ujenzi wa nyumba hizo inaonyesha kwamba mtu wa kawaida hatakuwa na uwezo wa kuzinunua kutokana na ukubwa wa bei jambo alilolieleza kuwa linaondoa maana halisi ya azma iliyokusudiwa na serikali yenyewe ama wananchi walalahoi.

No comments:
Post a Comment