AL AHLY KUIVUTIA KASI YANGA.

WAPINZANI
wa timu ya Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika, Al Ahly ya Misri
watakabiliwa na kibarua kigumu kesho wakati watakapokuwa wenyeji wa timu ya CS
Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa kugombea taji la Super Cup utakaofanyika
jijini Cairo. Al Ahly itabidi wasahau matokeo mabovu ambayo wamekuwa
wakipata katika mechi za ligi ya nyumbani msimu huu kama wanataka kuweka rekodi
ya kunyakuwa taji la Super Cup kwa mara ya sita.
Mechi hiyo ambayo huwakutanisha
mabingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita ambao ni Al Ahly na mabingwa wa
Kombe la Shirikisho ambao ni Sfaxien unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Taifa
wan chi hiyo uliopo jijini Cairo ambao una uwezo wa kubeba mashabiki
75,000.
Kocha wa Al Ahly Mohamed Youssef amesema anaamini mechi hiyo ni
muhimu kwao kwani itawasaidia wachezaji wake kuongeza kujiaminina kusahau
matokeo mabovu yaliyowaandama katika wiki za karibuni. Yanga tayari
imeshatuma shushu wake katika mchezo huo ambaye ni kocha msaidizi Charles
Boniface Mkwasa kwa ajili ya kuwapeleleza wapinzani wao hao kabla ya mechi yao
itakayochezwa Februari 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

KIUNGO
mahiri wa klabu ya Manchester United, Darren Fletcher ameitwa katika kikosi cha
timu ya Scotland kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Poland
mwezi ujao. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amerejea uwanjani hivi
karibuni kufuatia kuugua na anategemewa kuwepo katika mchezo huo utakaochezwa
jijini Warsaw Machi 5mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kuvaa jezi za Scotland
toka afanye hivyo mwaka 2012.
Fletcher ambaye ameichezea Scotland mechi
61, alieleza nia yake ya kutaka kurejea katika majukumu ya kimataifa mara baada
ya kupona. nYota huyo aligundulika kusumbuliwa na vidonda vya tumbo mwaka
2011 lakini amefanikiwa kurudi uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa
eneo lililoathirika.
WENGER.

MENEJA
wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa Bayern Munich bado haijafikia kiwango
cha Barcelona iliyonyakuwa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya chini
ya kocha Pep Guardiola. Arsenal watakuwa wenyeji wa mabingwa hao wa Ulaya
katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa barani
Ulaya leo usiku huku wakiwa na kumbukumbu ya kung’olewa katika hatua kama hiyo
na Bayern msimu uliopita sambamba na Barcelona ya Guardiola mwaka 2010 na
2011.
Ingawa Guardiola amekuwa kocha wa Bayern hivi sasa, Wenger bado
anaamini Barcelona ya kipindi kile bado ilikuwa bora kuliko Bayern ambao msimu
uliopita walishinda mataji matatu kwa mpigo. Wenger amesema alikuwa
akivutiwa zaidi na Barcelona ya kipindi kile kutokana na kasi ya pasi na mchezo
wao ni mategemeo yake hawatakutana na hilo watakapocheza na Bayern.

NGULI
wa soka wa klabu ya Bayern Munich, Stefan Effenberg anaamini kuwa Arsenal
inaweza kuwapa wakati mgumu mabingwa hao watetezi kama watatumia aina ya mchezo
wa kushambulia katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa baadae
leo. Arsenal watakuwa wenyeji wa Bayern inayonolewa na Pep Guardiola
katika Uwanja wa Emirates na kama wakiwafunga Wajerumani hao itakuwa timu ya
pili kuifunga Bayern toka Julai 2013.
Kulingana na wacheza mahiri kama
Mesut Ozil, Olivier Giroud na Santi Carzola waliopo katika kikosi cha Arsene
Wenger, Effenberg anaamini kuwa Arsenal inaweza kuwashangaza Bayern katika
mchezo huo. Effenberg amesema pamoja na ubora wa Bayern walionao lakini
bado wanaudhaifu katika safu yao ya ulinzi na kama Arsenal wakitumia vyema
nafasi zao wanaweza kuibuka kidedea katika mchezo huo ingawa bado anawapa
nafasi Wajerumani hao.
No comments:
Post a Comment