HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 16 February 2014

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: AZAM YATUPWA NJE HUKO BEIRA!


KIKOSI CHA AZAM FC


LEO HII, huko Beira, Msumbiji, Azam Fc ikicheza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, ilifungwa Bao 2-0 na Ferroviario de Beira na kutupwa nje kwa Jumla ya Bao 2-1.

Wiki iliyopita huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC iliifunga Ferroviario de Beira Bao 1-0.

Hapo Jana, Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Michuano hii ya Kombe la Shirikisho, Chuoni, walifungwa 2-1 Mjini Zanzibar na How Mine ya Zimbabwe na kutolewa kwa Jumla ya Bao 6-1 kwani Wiki iliyopita huko Zimbabwe walinyukwa Bao 4-0.

Timu nyingine ya Zanzibar inayocheza Michuano ya Afrika, kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI, ni KMKM ya Zanzibar ambao Leo huko Visiwani Zanzibar wanarudiana na Dedebit ya Ethiopia huku wakiwa nyuma kwa Bao 3-0 baada ya kuchapwa Wiki iliyopita huko Ethiopia.

Timu pekee ya Tanzania ambayo imefanikiwa kusonga kutoka Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI ni Yanga ambayo Jana hukO Comoro waliibonda Komorozine de Domoni Bao 5-2 na kuitupa nje kwa Jumla ya Bao 12-2 kwani waliifunga 7-0 Wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam.

Yanga sasa watacheza Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Al Ahly ya Misri ambao ndio Mabingwa Watetezi na Mechi hizi zitachezwa kati ya Februari 28 na Machi 2 na Marudiano ni kati ya Machi 7 na 9.
Kwenye Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho, Ferroviario de Beira watakutana na ZESCO ya Zambia.

No comments:

Post a Comment