DC wa Kilindi Suleiman Liwowa |
WAENDESHA
Boda Boda wilayani Kilindi mkoani Tanga wameiomba Mamlaka ya Mapato mkoani
Tanga (TRA)kuwapeleka wilayani humo huduma ya upatikanaji wa leseni kutokana na
vijana wengine kutokuwa nazo hali inayochangiwa na kutokwepo kwa ofisi
inayoshughulika na masuala hayo.
Kilio
hicho kilitolewa hivi karibuni na wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani hapa
wakati wakizungumza ambapo walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiikosa kitendo
ambacho kinawalazimu kusafiri mpaka Tanga mjini ili kufuata huduma hiyo
Evarist
Mosha mkazi wa kata hiyo na dereva wa bodaboda alisema kukosekana kwa huduma
hiyo wilayani humo serikali inakosa mapato kutokana na waendesha boda
boda wengi kutokuwa na leseni.
Akizungumzia
suala hilo,Mkuu wa wilaya ya Kilindi,DC wa Kilindi Suleiman Liwowa alisema ni
kweli katika wilaya hiyo hakuna ofisi za mamlaka ya mapato (TRA) na kutaka
uwekwe utaratibu ambao utawafikia wananchi na endapo watakubaliana nao wataweka
mazingira mazuri ya upatikaji ofisi.
No comments:
Post a Comment