Na Hafidh Kido Afisa Habari wa Coastal
Union
Ndugu zangu,
WIKI
hii kumekuwa na habari za upotoshaji juu ya kutimuliwa kwa kiungo mshambuliaji
wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, Haruna Moshi ‘Boban’.
Ninaziita
habari za upotoshaji kwasababu hazina ukweli, na mara nyingine mtu anaweza
kuenda mbali zaidi na kufikiri kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya timu yetu
ili wachezaji wasicheze kwa moyo wakati wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza Januari 25 mwaka huu.
Haruna Moshi, akimiliki mpira katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akiitumikia CUSC kwenye mechi yake
ya kwanza ligi kuu na Wagosi wa Kaya. Ilikuwa ni mechi dhidi ya Oljoro JKT,
ambapo CUSC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
|
Gazeti
moja la michezo, jina tunalihifadhi limeripoti likimnukuu kiongozi mmoja wa
Wagosi wa Kaya, jina pia tunalihifadhi kutokana na heshima yake; kuwa Coastal Union
haina mpango wa kumuongezea mkataba ‘Boban’ baada ya kumalizika miezi sita
ijayo kwasababu za utovu wa nidhamu.
Habari
hizo hazina ukweli kwasababu hakuna kikao kilichokaliwa kujadili mustakabali wa
mchezaji huyo. Ni kweli Boban, hajaripoti kambini mpaka sasa; lakini uongozi wa
juu akiwemo meneja wa timu unazo taarifa za mchezaji huyo.
Kuwa
na nidhamu ama kutokuwa na nidhamu, kumtimua ama kumuacha mchezaji, wanaoamua
hayo ni uongozi wa juu kupitia kamati zake ndogondogo kama za mashindano,
usajii na nidhamu. Na si mtu mmoja mmoja.
Hivyo
kwa niaba ya Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu inaomba
radhi wanachama wa CUSC, kutokana na kuumizwa kwa namna moja ama nyingine na
taarifa hizo za upotoshwaji.
Wagosi
wa Kaya, bado wana mkataba wa miezi sita na Boban, kuongezewa ama kutoongezewa
mkataba suala hilo litajadiliwa kati ya mchezaji na viongozi pale utakapofika
ukingoni.
HAFIDH
A. KIDO
MSEMAJI
CUSC
JANUARI
1, 2014
DAR
ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment