HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 3 January 2014

REA SASA KUSAMBAZA UMEME WILAYA SITA MKOANI TANGA.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa


Na Oscar Assenga,Tanga.

WAKALA wa nishati ya Umeme Vijijini (REA)unatarajiwa kukamilisha miradi ya Umeme katika vijiji mbalimbali mkoani Tanga ambapo ikikamilika itaongeza huduma  hiyo kwa wananchi na wawekezaji waliopo kwenye maeneo yao hali ambayo itachangia kasi maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa aliyasema hayo hivi karibuni wakati akitoa taarifa ya mafanikio kwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi Octoba 2013 ambapo alisema kwenye mpango  huo jumla ya wilaya sita zitanufaika.

Gallawa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013-2014 wakala umepanga kupeleka umeme katika maeneo ya wilaya ya Handeni kwenye vijiji vya Kideleko,Kigombe, Madebe,Nyasa na Gole ili kuwawezesha wananchi hao kufaidika na huduma ya nishati.

Alisema kwenye wilaya ya Korogwe mji wakala wa nishati ya umeme vijiji watapeleka kwenye maeneo ya Maili Kumi,Taasisi ya Utafiti ya Tafori,Kwamgwe, Jambe,Kamsisi, Kwamndolwa, Kwakombo,Kwameta, Kwange,Msambiazi, Darajani,Gereza, Kwamzindawa,Mgobe, Kituo cha Afya Kwalukonge,Miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji ya Kitivo na Mombo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema katika wilaya ya Lushoto vijiji ambavyo vitanufaika na mradi huo ni eneo la Mlola kupitia vijiji vya Mnadani,Mtumbi,Mshangai,Kwekanga na Mathego wakati wilaya ya Mkinga watapeleka umeme vijiji vya Manza Bay,Daluni na Gombero.

Aidha aliitaja eneo lengine ambalo litafaidika na huduma hiyo ni Korogwe Vijijini ambapo wakala atapelekea nishati hiyo kwenye vijiji vya Malibwi, Manolo, Hambogo, Ngwelo,Dindira, Kijungumoto,  Kijango,Lusanga,Kwamazandu ,Makumba, Mkwakwani,Vugiri,Makose,Nkalai,Sunga,Kihitu,Malindi na Rangwi.

Katika wilaya ya Pangani wakala watapeleka umeme katika vijiji viwili ambavyo ni Mkalamo na Mbulizaga ambapo ukamilikaji wa miradi hiyo utasaidia wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kupata nishati hiyo bila kikwazo.

No comments:

Post a Comment