Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa |
Tanga.
HALI
ya uvunaji wa mazao ya baharini katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka
tani 481 zilizopatikana mwaka 2011/2012 zenye thamani ya fedha za kitanzania
4,821,440,915.15 zilizosafirishwa nje ya nchini hadi kufikia tani 316 kwa mwaka
2012/2013 ambapo upungufu huo wa tani 165.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa wakati
akizungumza na wanahabari ambapo alisema upungufu huo umesababishwa na
hali ya soko la mazao kama Pweza kwa nchi Ulaya kupungua.
Gallawa
alisema sekta ya uvuvi mkoani Tanga imeendelea kutunza mazingira ya uzalishaji
wa mazao ya majini kwa kudhiti uvuvi haramu ambapo mwaka 2011-2012 jumla
ya doria 120 zilifanyika na kufanikiwa kuwakamata wahalifu 20 na
kuwafikisha mahakamani.
Licha
ya kuwakamata watuhumiwa hao pia walikamata vyombo vya baruti 6 na baruti
10 na bunduki 5 za kuvulia zilikamatwa,Samaki wa baruti kilo 240 walikamatwa na
kutekelezwa na makokoro ikiwemo juya 60 ambavyo vilikuwa vikitumika
kwenye uvuvi haramu.
Aidha
alisema jumla ya kesi 22 zilifuatiliwa mahakamani ambapo kesi CC 06/2009
inayohusu mtu mmoja kwa kosa la kupatikana na samaki wa baruti ilitolewa hukumu
ya kifungo cha miezi mitatu jela na kesi CC 363/09 inayohusu mtu mmoja
kupatikana na samaki w baruti iliyotolewa hukumu ya kumuachia huru mshtakiwa
wakati kesi nyengine zilikuwa zikiendelea.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka 2012-2013 Jumla ya doria 44
zilifanyika na kesi 10 zilifuatiliwa mahakamani ambapo jumla ya vyombo vya
baruti 20 vilikamatwa pamoja na sanmaki wa baruti 160 walikamatwa.
Aliongeza
kuwa pia magari 20 yanayosafirisha mazao ya samaki kwenda mikoa mbalimbali
yalikaguliwa ambapo kwenye mwaka huu mikuki,mishale ya kuchomea samaki 20
ilikamatwa ikiwemo makokoro na juya 5 zilikamatwa.
Soko la Deep Sea Eneo Maarufu kwa Uuzaji wa Samaki jijini Tanga |
No comments:
Post a Comment