Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kushoto akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa
Mapinduzi, Nahodha wa KCC ya Uganda, Fahad Kawooya jioni ya leo Uwanja wa
Amaan, baada ya kuifunga Simba SC 1-0.
|
BAO pekee la Herman Wasswa, limeipa KCC ya Uganda ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2014, baada ya kuilaza Simba SC 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni hii.
Waswa alifunga bao hilo dakika ya 20 baada ya kumhadaa beki wa kushoto wa Simba SC, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na kufumua shuti lililompita kipa Ivo Mapunda aliyekuwa amezubaa.
Unaweza
kusema lilikuwa bao rahisi, kwa sababu kipa Ivo aliamini Baba Ubaya atamdhibiti
Wasswa, lakini badala yake beki huyo akampa mfungaji mwanya wa kupiga ghafla.
Pamoja na
kurejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba
SC walicheza vizuri isipokuwa bahati haikuwa yao.
Safu ya ulinzi ya KCC ilikuwa imara mno leo kuwadhibiti washambuliaji wote wa Simba SC hadi mwisho wa mchezo.
Kipindi cha
pili, Simba SC ingeweza kufungwa bao la pili kutokana na wachezaji wake wote kwenda
kushambulia na KCC wakawa wanatumia nafasi hizo kufanya mashambulizi ya
kushitukiza yaliyokuwa hatari.
Lakini nao
Simba SC katika kushambulia kwao walikosa mabao ya wazi kutokana na
washambuliaji wake kukosa umakini katika kumalizia nafasi nzuri walizotengeneza.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein alimkabidhi Kombe la ubingwa wa Mapinduzi na fedha taslimu, Sh. Milioni 10, Nahodha wa KCC, Fahad Kawooya.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein alimkabidhi Kombe la ubingwa wa Mapinduzi na fedha taslimu, Sh. Milioni 10, Nahodha wa KCC, Fahad Kawooya.
Simba SC
walipewa Sh, Milioni 5 kwa kushika nafasi ya pili, wakati mchezaji Tony Odur wa
KCC alipewa king’amuzi cha Azam TV kwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Mkurugenzi wa CXC Safaris & Tours ya Dar es Salaam, Charles Hamkah alikabidhi Sh. 300,000 kwa kila mmoja, mfungaji bora Owen Kasuule wa URA, mchezaji bora Mwinyi Mngwali wa Cloves Stars na kipa bora, Ivo Mapunda wa Simba SC.
Mkurugenzi wa CXC Safaris & Tours ya Dar es Salaam, Charles Hamkah alikabidhi Sh. 300,000 kwa kila mmoja, mfungaji bora Owen Kasuule wa URA, mchezaji bora Mwinyi Mngwali wa Cloves Stars na kipa bora, Ivo Mapunda wa Simba SC.
Kwa kutwaa
ubingwa huo, KCC inakuwa timu ya kwanza kutoka nje ya Tanzania kubeba taji hilo
na bingwa wa nane kihistoria wa Kombe la Mapinduzi.
Sasa ni timu
sita zimetwaa Kombe hilo tangu limeanzishwa mwaka 2007, Yanga SC ya Dar es
Salaam ikikata utepe, ikifuatiwa na watani wao, Simba SC (2008), Miembeni ya
hapa (2009), Mtibwa Sugar ya Morogoro (2010), Simba SC tena 2011 na Azam FC
mara mbili mfululizo 2012 na 2013 na KCC mwaka huu.
Mabingwa
watetezi, Azam safari hii wamekwamia kwenye Nusu Fainali baada ya kutolewa na
KCC kwa kufungwa mabao 3-2, ikitoka nyuma kwa 2-0.
Kikosi cha
Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/William Lucian ‘Gallas’, Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’/ Uhuru Suleiman,, Donald Mosoti ‘Beki Adui’, Joseph Owino,
Jonas Mkude/Said Ndemla, Haroun Chanongo/Betram Mombeki, Amri Kiemba, Amisi
Tmbwe, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Awadh Juma/Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
KCC; Omar
Magoola, Saka Mpima, Habib Kavuma, Ibrahim Kiiza, Fahad Kawooya, Gadafi
Kiwanuka, Herman Wasswa, Tom Masiko, Tony Odur, Stephen Bengo na William
Wadri/Hakim Serukumba.
No comments:
Post a Comment