MALINZI
KUTEMBELEA KITUO CHA ALLIANCE
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafanya ziara ya
siku moja kutembelea kituo cha mpira wa miguu wa vijana cha Alliance cha jijini
Mwanza.
Lengo
la ziara hiyo ni kuangalia jinsi Alliance inayoendesha shughuli zake ili Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liweze kushirikiana na kituo hicho kwa karibu.
Rais
Malinzi katika ziara hiyo atakayoifanya keshokutwa (Januari 15 mwaka huu)
atafuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu kwa Vijana, Ayoub Nyenzi
na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ramadhan Nassib.
Alliance
inatarajia kufanya mashindano yatakayoshirikisha vituo vyote vya kuendeleza
mpira wa miguu kwa vijana (academy) wiki ya tatu ya Februari mwaka huu jijini
Mwanza.
Mashindano
hayo yatashirikisha timu za umri wa miaka 13, 15 na 17 ambapo Alliance
itagharamia malazi, chakula na usafiri wakati timu hizo zikiwa jijini Mwanza.
YAHYA
KUFUNGA SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Hamad Yahya atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa semina ya waamuzi na
makamisha.
Semina
hiyo ya siku mbili itafungwa kesho (Januari 14 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye
ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
zaidi ya 100 na makamishna 50 wanashiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni
baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja
la Kwanza (FDL).
Kwa
upande wa waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo
wanaochezesha mechi za VPL na FDL.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine baadaye
mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.
VITAMBUSHO
KWA WAANDISHI WA MPIRA WA MIGUU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa vitambulisho vipya kwa waandishi wa
habari za mpira wa miguu kwa ajili ya kuripoti mechi mbalimbali inayoziandaa na
kuzisimamia.
Kila
chombo cha habari kupitia Mhariri wake au Mhariri wa Michezo kinatakiwa
kuwasilisha majina ya waandishi wake kwa barua maalumu ya ofisi pamoja na picha
(soft copy) kwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Orodha
ya majina ya waandishi wakiwemo wapiga picha wanaoombewa vitambulisho hivyo
iwekwe kwa umuhimu.
RAMBIRAMBI
MSIBA WA MCHEZAJI BONIFACE NJOHOLE
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa
zamani wa timu ya Reli Morogoro, Boniface Njohole kilichotokea jana (Januari 12
mwaka huu) mkoani Morogoro.
Njohole
ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) hadi umauti unamkuta anatarajia kuzikwa kesho
(Januari 14 mwaka huu) kijijini kwao Mngeta wilayani Ifakara.
Msiba
huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani alitoa mchango akiwa mchezaji,
kocha na kiongozi kwa nyakati tofauti, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Njohole, klabu ya Reli na MRFA na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia
TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
No comments:
Post a Comment