HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 15 January 2014

JESHI LA POLISI MKOANI TANGA LAKUSANYA SH MIL 801.8 KWA MAKOSA YA BARABARANI 2012-2013



Tanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga Kitengo cha Usalama barabarani, limeongeza makusanyo yanayotokana na makosa mbalimbali, kutoka Sh milioni 738.2 hadi kufikia Sh milioni 801.8. Ongezeko hilo ni la kuanzia mwaka 2012 na 2013, fedha ambazo zilitokana na makosa mbalimbali ya barabarani, baada ya uimarishwaji wa doria kwenye barabara kuu na za mijini.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Isango akizungumza na daadhi ya BodaBoda katika semina iliyotolewa jijini Tanga mwaka 2013
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Isango aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alisema fedha hizo zilikusanywa kutokana na makosa 26,178 yaliyopatikana mwaka jana na makosa 24,160 yaliyopatikana mwaka juzi.

Isango alisema makosa mengi yanatokana na ubovu wa matairi, kutokufunga mikanda na uendeshaji mwendo kasi ambao mara nyingi husababisha ajali na kupoteza maisha ya raia wasiokuwa na hatia kwa madereva wanaotumia barabara za Mkoa wa Tanga.

Aidha alisema takwimu za ajali za barabarani zimeonekana kupungua kwa kiasi kidogo, kutoka ajali 98 zilizojitokeza mwaka jana zilizosababisha majeruhi 219 ikiwemo watu 129 kufariki dunia kutokana na ajali hiyo, wakati mwaka juzi zilitokea ajali 98 zilizoua watu 104 ambapo ongezeko hilo ni sawa na vifo 25, ambayo ni sawa na asilimia 24 pamoja na majeruhi 153 ikiwa ni ongezeko la asilimia 66.

Akizungumzia ajali za pikipiki kati ya mwaka 2012-2013, Isango alisema ajali hizo zimepungua kutoka vifo 24 mpaka kufikia vifo 21, ambavyo ni sawa na ongezeko la asilimia 12.5 ambapo punguzo hilo limetokana na waendesha pikipiki wengi kupata elimu ya usalama barabarani na uimarishaji wa doria kwenye barabara kuu zote mkoani hapa.

Aliwataka wananchi kuacha kuendelea kutoa rushwa, kwa sababu kuendelea kufanya hivyo kunaweza kusababisha ongezeko la ajali za mara kwa mara barabarani, kwani wanapokuwa wakitoa rushwa askari wanashindwa kuwajibika ipasavyo na kuyaacha magari kuendelea na safari zake bila kujali madhara yatakayoweza kuwakuta.

No comments:

Post a Comment