MKUU WA WILAYA HANDENI, MKOANI TANGA, MUHINGO RWEYEMAMU
|
HALMASHAURI
ya Mji wa Handeni, imepitisha mapendekezo ya bajeti yake ya mwaka 2014-2015 ya
jumla ya kiasi cha sh. bilioni 7.9 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo
fedha za utawala kwa watendaji.
Akisoma
mapendekezo hayo katika baraza la madiwani la halmashauri ya mji huo mwishoni
wa wiki, Kaimu Mwekahazina wa mji huo, Npella Kwidika amesema mapendekezo ya
bajeti hiyo imezingatia mipango, sera na ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 na
kwamba wamelenga kupata fedha hizo kwenye vyanzo vyao vya mapato na ruzuku toka
Serikali Kuu.
Amesema makusanyo ya ndani wamepanga kukusanya kiasi cha sh. milioni 720 fedha zitakazolipa mishahara kwa watumishi ni sh. bilioni 5.9 ruzuku na matuminzi sh. milioni 709 huku miradi ya maendeleo wakiwa wamepanga kutumia kiasi cha sh. milioni 503.
Mwekahazina huyo pia amesema kwamba nje
ya bajeti hiyo, wameomba hazina kiasi cha sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya
ujenzi wa jengo la utawala ambalo litagharimu kiasi cha sh. bilioni 1.5 fedha
za kujenga maabara za shule za sekondari zipatazo nane zilizopo katika
halmashauri hiyo kiasi cha sh. milioni 624 huku wakipanga kiasi cha sh. milioni
250 kwa ajili ya magari ya mkurugenzi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa halmashauri
hiyo, Thomas Mzinga amesema kwenye kikao hicho kwamba wamepanga kukusanya kiasi
cha shilingi milioni 200 kutoka katika kodi ya majengo katika mji huo utaratibu
ambao unatarajiwa kuanza januari 15 mwaka huu na kwamba wananchi wote
wametakiwa kulipa fedha hizo.
No comments:
Post a Comment