Kikosi cha Yanga salama kiliwasili nchini Uturuki hapo jana Usiku ambapoMara baada ya kuwasili katika hoteli ya Sueno Beach Side eneo la Manavgat pembeni kidogo ya jiji la Antalya kikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kimataifa barani Afrika.
Timu ilipokelewa na wenyeji majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za huku ikiwa ni sawa na saaa 12 kwa saa za Afrika Mashariki na moja kwa moja kikosi kilielekea katika mji wa Manavgat ambapo ndipo ilipo hoteli ya Sueno Beach Side ambapo msafara mzima umefikia.
Robert Carlos kocha wa
Sivasspor na mchezaji wa zamani wa timu ya Real Madrdi na timu ya Taifa Brazil
(katikati) akiwa na wachezaji na viongozi wa timu ya Young Africans katika
picha ya pamoja
|
Sueno Hotel Beach Side ni hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano, ambayo ina jumla ya vyumba 760, mabwawa ya kuogelea,viwanja viwili vya mpira vya mazoezi kimoja kikiwa na nyasi za kawaida na kingine nyasi za bandia.
Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru kikosi chake kimefika salama na wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya na kifikra hivyo anatarajiwa mazoezi yatakayoanza leo yatasaidia kuiweka timu katika hali nzuri na kuwa tayari kwa mashindano.
"Kazi yangu kubwa ni kukiandaa kikosi kiwe katika hali nzuri ili pindi tutakaporejea nchini timu iwe fiti na tayari kwa ajili ya mashindano, kwa hali ilivyo nzuri na mazingira naamini timu itabadilika na kurejea nchini ikiwa katika kiwango cha kizuri cha ushindani" alisema Mkwasa
Young Africans inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini Uturuki.
Robert Carlos kocha wa Sivasspor na mchezaji wa zamani wa timu ya Real Madrdi na timu ya Taifa Brazil (katikati) akiwa na wachezaji na viongozi wa timu ya Young Africans katika picha ya pamoja
Aidha timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki inayonolewa na mchezaji wa zamani Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil Roberto Carlos pia imeweka kambi katika hoteli ya Sueno na leo asubuhi kabla ya Young Africans kuanza mazoezi waliweza kupiga picha ya pamoja na gwiji huyo.
Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini katika
viwanja vya Sueno Hotels Beach Side eneo la Manavgat – Antalya
|
No comments:
Post a Comment