HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 9 January 2014

NOAH YAUA WAWILI MKATA NA KUJERUHI NANE



na oscar assenga, handeni.
Watu wawili wamefariki dunia hapo hapo na wengine nane kujeruhiwa  baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wamepanda kutaka kulipita gari lililkuwa mbele yake na kukutana na gari lori aina ya volvo na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa tanga,Costastine Massawe   athibitisha kutokea tukio hilo leo na kueleza tukio hilo lilitokea majira ya saa tano mchana wakati gari hilo aina ya noah t266 axz lililokuwa likitokea kabuku kwenda mkata ambapo lilipofika eneo la kwamgogo ndio lilipotaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na ndipo alipkutana na
lori aina ya Volvo na kugongana nalo.

Massawe amtaja dereva wa gari aina ya Noah aliyesababisha ajali hiyo kuwa ni abdallah selehe (60) mkazi wa kata ya hale wilayani Korogwe mkoani tanga ambaye alikimbizwa kwenye hospitali ya mkata handeni
akiwa hajitambui akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

Aliwataja watu waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni wanawake wawili ambao walikuwa miongoni mwa abiria waliokuwepo kwenye gari hilo aina ya Noah ambapo kwa mujibu wa kamanda masawe majina yao haya kuweza kupatikana mara moja.

Kamanda massawe alisema chanzo cha ajili hiyo ni dereva za gari hilo aina ya noah kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake kwenye kona na ndipo ambapo alipokutana uso kwa uso na lori hilo na kusababisha ajali
hiyo.

"ajali nyingi zinatokea kutokana na madereva kutokuwa makini kwani wengi wao wanasababisha ajali hizo kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yao bila kufikiria kufanya hivyo ni kukiuka sheria za usalama barabarani "alisema kamanda massawe.

Aidha kamanda  massawe alitoa wito madereva mkoani tanga kutii sheria bila shuruti kwa kufuata sheria za usalama barabarani na kuwataka abiria kuacha kushabikia mwendokasi badala yake watoe taarifa kwa jeshi hilo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment