Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa |
Na
Oscar Assenga, Tanga.
JUMLA
ya wahamiaji haramu 590 walikamatwa mkoani Tanga katika kipindi cha
kuanzia Januari 2012 hadi octoba 2013 kutokana sababu mbalimbali ikiwemo
kuingia nchini bila kibali na kufanya kazi.
Takwimu
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati
akitoa taarifa ya mafanikio ya mkoa wa Tanga mwaka 2012 hadi Octoba 2013 kwa vyombo
vya habari mwishoni mwa wiki.
Gallawa
alisema kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2012 jumla ya watuhumiwa 289
wa mataifa ya Ethiopia 116,Kenya 53,Uganda 29,Switzerland 1,India 6,Italia
1,German 4,Afrika Kusini 3,Somalia 18,Portugues 1,Bangladesh 2,Denmark 1,Zambia
2,China 2,Congo1.
Aidha
aliongeza kuwa wahamiaji haramu waliokamatwa kutoka mataifa mengine ni Guinea
1,Turkey 1,Sri-Lanka 1,Pakistan 6,Peru 1,Egypt 1,Norway 2 na watanzania
32 ambao walikamatwa kwa makosa yaliyotajwa hapo juu ukilinganisha na kipindi
cha kuanzia Januari hadi Octoba 2013 ambapo jumla ya watuhumiwa 301
kutoka nchi mbalimbali waliokamatwa.
Gallawa
alisema katika kipindi hicho wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia 213,Kenya
29,India 9,China 3,Bangladesh 7,Djibout 1,Pakistan 1,Burundi 1,Somalia
2,British 2,Osterech 1,Uganda 2,Israel 2,USA 2 na watanzania 25.
Aliongeza
kuwa takwimu hizo zinaonyesha idadi ya wahamiaji haramu hasa raia wa Ethiopia
waliokamatwa imeongezeka kati ya mwaka 2012 hadi kufikia Octoba 2013 .
Mkuu
huyo wa mkoa alisema idadi ya watanzania waliokamatwa kwa kosa la kusaidia au
kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji haramu imepungua ukilinganisha na
kipindi cha mwaka 2012.
Alisema
takwimu hizo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa idara ya uhamiaji Tanga
kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari zitokanazo na wahamiaji haramu na
ushirikishwaji wa wananchi dhidi ya mapambano ya kudhibiti wimbi la wahamiaji
haramu nchini.
Hatua
zilizochukuliwa dhidi ya wahamiaj haramu hao ni kufikishwa mahakamani pamoja na
kufukuzwa nchini kwa kupewa notisi.
No comments:
Post a Comment