Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costantine Massawe(Picha na Maktaba) |
Korogwe
Watu watano wanaodhaniwa kuwa majambazi
wamekamatwa na polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa tuhuma za kukutwa na
bunduki aina ya Shortgun na sare za polisi wakati wakijiandaa kwenda kufanya
uhalifu .
Akithibitisha
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costantine Massawe alisema
majambazi hao wamekamatwa Kijiji cha Gomba Kata ya Makuyuni wilayani hapa
Desemba 28 mwaka 2013 saa 4:00 usiku baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria
mwema .
Kamanda
Massawe alisema bunduki hiyo iliyokuwa na risasi tatu, ina namba ya Model-1400
MK II ambayo Taratibu Hemed ndiye anayeimiliki kihalali, lakini amekuwa
akiikodisha kwa majambazi na kuletewa fedha anazotumia kulipia kibali cha
silaha hiyo.
Massawe
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Zacharia Jeras {50] Mkazi wa Makanya Same
Kilimanjaro , Mosses Jonasi {44} na Selemani Jaha {21} wote wakiwa wakazi wa
Makanya Same mkoani Kilimanjaro ambapo walikiri kwenda kufanya uhalifu katika
kijiji hicho cha Gomba.
Alitaja
watuhumiwa wengine kuwa ni Taratibu Hemedi{74} ambaye ni mmiliki wa silaha hizo
na sare pamoja na Hemedi Taratibu {32} ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa anayemiliki
silaha hizo na sare hizo ambazo ni za polisi.
Kamanda
huyo alisema polisi inaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa
mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
No comments:
Post a Comment