Na Oscar Assenga,Tanga.
KATIBU wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema chama hicho kitahakikisha
kinawapitisha wagombea wanaokubali kwenye chaguzi za udiwani na wenyeviti wa
serikali za vijiji ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika mikoa ya
Tanga ,Kilimanjaro na Arusha kuziba nafasi zilizoachwa wazi lengo likiwa ni
kushika hatamu ya uongozi kwenye chaguzi hizo.
Golugwa alisema hayo leo wakati
akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema mikakati hiyo itakwenda sambamba na
ufanyaji wa kampeni za kiustarabu kwa kueleza sera makini ambazo zitawapa
hamasa wananchi kuweza kukichagua chama hicho lengo likiwa kuwapa maendeleo
pamoja na kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili.
Alisema umuhimu wa kuwaweka wagombea
wanaokubali kwenye chaguzi hizo ni mkubwa sana kutokana na kutaka kutengeza
historia ya kipekee kwa kuwa na madiwani wawili kwenye jimbo la Tanga ambao
wataweza kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa viongozi wengine waliopo.
“Chama chetu kitaingia kwenye mchakato
wa kuangalia nani anaweza kuipeperusha bendera kwenye chaguzi hizo na ambaye
atakuwa akikubalika kwa asilimia kubwa na wananchi wa mahala husika na sio
vyenginevyo “Alisema Bolugwa.
Alisema kuelekea uchaguzi huo lazima
wanachama na wapenzi wa chama hicho kuachana na makundi ambayo hayana tija kwao
badala yake kuwa na mshikamano ambao utawawezesha kupata mafanikio ambayo
yanapeleka kushika nyazifa za uongozi kwenye kata na vijiji hivyo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika
kutokana kata mbili mkoani Tanga ambazo ni Kiomoni na Mtae Jimbo la Mlalo
wilayani Lushoto viongozi wao kutokuwepo kwa kufariki na kujiuzulu na hivyo
kupelekea nafasi zao kubaki wazi.
Aliyataja maeneo mengine yaliyowazi ambapo
uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika ni kata ya Sombeni Jimbo la Arusha,Kata ya
Kiboroloni Jimbo la Moshi na Karachimbi Jimbo la Kiteto Manyara.
No comments:
Post a Comment