Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Hemed Aurora(kulia)akipokea kombe la uhai |
UONGOZI wa Klabu ya Coastal
Union ya Tanga umemwagia sifa Kocha mkuu wa timu hiyo Yusuph Chipo kutokana na
uwezo wake kiutendaji alioufanya kwa kipindi kifupi ambacho amekabidhiwa timu
hiyo ambacho kinaonyesha mafanikio makubwa kwao siku za mbeleni.
Akizungumza jana,Mwenyekiti wa Klabu ya
Coastal Union ya Tanga,Hemed Aurora “Mpiganaji”alisema uwezo wa mwalimu huo
umeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa timu yao ya pili kuweza kuchukua ubingwa wa
kombe la uhai Cup na kuweza kuipa heshima timu hiyo na mkoa wa Tanga kwa
ujumla.
YUSUPH CHIPO(KULIA) |
Aurora alisema kilichofanywa na kamati
ya utendaji kwa kuamua kumuondoa aliyekuwa kocha wao Hemed Moroco kilikuwa ni
sahihi na cha kizalendo ambacho leo hii kimeweza kuleta mapinduzi makubwa
na maendeleo ya timu yao hasa kikosi cha pili.
Alisema kutokana na uwezo wake wana
imani kubwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara wataweza kufanya vizuri
kutokana na kocha huyo kupewa kila anachokitaka na mshikamano uliopo
baina wa wapenzi viongozi na wanachama wao.
Mwenyekiti huyo alisema kabla ya kuanza
mzunguko wa pili wa ligi kuu wanatarajiwa kuweka kambi ya wiki mbili Maskati
nchini Omani ambayo itakuwa na lengo la kukipa makali kikosi chao ambacho
kinakabiliwa na michezo yao ligi hiyo.
Alisema wakiwa nchini Omani
wanatarajiwa kucheza mechi nne za kirafiki ambapo hilo linategemea na ratiba ya
wanyeji wao timu ya Finya FC ya Omani ambayo inashiriki ligi kuu nchini humo.
Wakati huo huo,Aurora alioupongeza
uongozi mpya wa shirikisho la soka nchini (TFF)chini ya Rais wake Jamali
Malinzi na Makamu wake Walece Karia kwa kuchaguliwa kuongoza shirikisho
hilo na kueleza kuwa anaamini watakuwa chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu
hapa nchini.
KIKOSI
CHA COASTAL UNION
|
No comments:
Post a Comment