NA RAMADHANI JUMA,
OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO
MKUU wa mkoa
wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapa
pamoja na taasisi nyingine za serikali kutotoa kazi yoyote ya ujenzi kwa
kampuni ya ujenzi ya ‘Juin Constructions Company Limited ’ kutokana na kampuni
hiyo kuonekana kufanya kazi zake chini ya kiwango.
Alitoa
maamuzi hayo wakati alipokuwa akikagua jengo la bweni la wasichana linalojengwa
katika shule ya sekondari ya Kasanga iliyopo kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo
Mkoani Rukwa .
Alisema
wakandarasi wengi wamekuwa wakiihujumu mikoa ya pembezoni mwa nchi ukiwemo Mkoa
wa Rukwa kwa kujenga miradi isiyo na viwango kwa muda mrefu sasa, na kwamba
umefika wakati wa kupambana na hali hiyo.
Aliagiza
kampuni hiyo iwekwe kwenye orodha ya makampuni yasiyotakiwa kupewa kazi
katika mkoa wa Rukwa mara moja ili iwe fundisho kwa makampuni mengine
yanayolipwa fedha za umma kwa kazi zilizo chini ya kwango.
Mbali
kutekeleza jengo hilo chini ya kiwango, Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema
mkandarasi huyo amekuwa hafuati ushauri wa wataalam wa Halmashauri ya Kalambo
iliyompa kazi hiyo.
“Mkandarasi
huyu hajawahi kupatikana katika eneo la mradi wakati wa ukaguzi hata siku
moja..kila mara wakaguzi wakitembelea mradi huu yeye huwa hayupo kwahiyo huyu
hatufai katika mkoa wetu” alifafanua.
Kwa upande
wake mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Issa Liyanga
alisema wamekuwa wakimsimamia mkandarasi huyo katika hatua mbalimbali za ujenzi
wa jengo hilo ambapo hata hivyo amekuwa na ushirikiano hafifu katika kuzingatia
ushauri unaotolewa.
No comments:
Post a Comment