Na Oscar Assenga,Tanga.
MSANII wa
muziki wa Bongo Fleva Mkoani Tanga,Ally Khamisi "Dullah wa Michano"apania
kuendelea mziki wa kizazi kipya mkoani hapa kwa kuwakutanisha wasanii hao lengo
likiwa kuinua vipaji vyao.
Dulla wa Michano |
Dulla wa
Michano alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wanahabari ambapo alisema bila jitihada na sapoti kubwa
kwa wasanii ikiwemo kushirikiana mziki huo hauwezi kufika mbali hivyo lazima
wasanii wakubali kuwa na mshikamano ili kuweza kuleta mapinduzi katika tasnia
hiyo.
Michano
ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake
"NAZEEKA"aliomshirikisha kaka yake SELLE wa MICHANO amsema ana
matumaini makubwa utafanya vizuri kama nyengine zilizopita ambavyo pia
zinaendelea kuubamba mziki wa bongo fleva hapa nchini.
Wimbo huo
aliurekodia kwenye studio za DIVA TALENT inayomilikiwa na MESEN SELECTA ambapo
ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimemtambulisha sana kwenye mziki huo ambao
umeonekana kuwa na wapenzi wengi hapa nchini.
Akizungumzia
mziki huo,alisema mziki wa bongofleva unalipa kilichobakia ni watu kuwa makini
na kujitambua wanapaswa kufanya nini ili kuweza kuendana na ushindani.
"Kama
unavyojua mziki wa sasa unalipa tofauti na miaka ya nyuma hivyo wasanii
wanapaswa kutumia umakini mkubwa hasa wakati wanapokuwa wakitunga mashairi yao
na sio kukurupuka kitendo ambacho kinawapeleka kushuka badala ya kupiga hatua
za kimaendeleo "Alisema Dulla wa Michano.
Aidha
aliwataka watangazaji na watayarishaji wa mziki huo kuwapa nafasi wasanii
wachanga ili nao waweze kuonyesha vipaji vyao badala ya kuwabania kwani kufanya
hivyo kunapeleka kushuka mziki huo.
No comments:
Post a Comment