DC wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego |
WILAYA ya Tanga katika mwaka huu wa
2013 mefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa ufaulu wa wanafunzi
wa darasa la saba ambao walifanya mtihani wao wa Taifa mwezi wa kumi
ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.
Akizungumza ofisini kwake kaimu Afisa
elimu Jiji, Damas Kifanga alisema kuwa ufaulu huo uliojumuisha shule 93 za
Tanga mjini na Vijijini umeongezeka mwaka huu ingawa sekta hiyo ya elimu
inakabiliwa na changamoto nyingi.
Aidha alisema katika sekta hiyo ya
elimu Wilaya ya Tanga mwaka huu imefanikiwa kutoa wanafunzi 4266 kati ya
wanafunzi 6261 sawa na 40% ya ufaulu wa matokeo ya darasa la saba ambapo ni
tofauti na mwaka jana kitu ambacho kinaleta hamasa katika sekta hiyo muhimu
katika maisha ya kila siku.
Hata hivyo Kifanga alisema kuwa ili
kukabiliana na idadi ndogo ya wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na shule
za serikali,ni lazima kuunganisha nguvu kutoka serikalini,wazazi na taasisi
zisizo za kiserikali ili kuweza kuinua sekta hiyo ya elimu katika Wilaya ya
Tanga Mjini.
Alisema kuwa
upo umuhimu wa utolewaji wa chakula mashuleni ili kuboresha mahudhurio na
kuwepo na usikivu mzuri wa wanafunzi pindi wawapo madarasani kitu ambacho bado
kinasuasua kwa baadhi ya shule na kupelekea kufikia malengo mazuri
waliojiwekea.
Kifanga alizidi kusema kuwa uboreshwaji
wa mindombinu ni muhimu katika sekta hiyo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi
katika baadhi ya shule kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kinaweza
kupunguza umakini kwa wanafunzi wawapo katika masomo yao.
Bwana Kifanga alitumia fursa hiyo
kuiomba serikali kuongeza jitihada katika utowaji wa fedha za uwendeshaji wa
shughuli zote za elimu na kuwa saidia kukamilisha kwa wakati miundombinu
amabyo wananchi wanayanzisha kwa nguvu zao katika kuboresha elimu Wilayani
humu.
Ameiomba serikali kuwa
Halmashauri zinapaswa kuboreshewa uewzo wa kifedha ili kuweza
kusaidia mafunzo ya walimu waliopo makazini ili waweze kutekeleza majukumu yao
kwa ufanisi zaidi wa kielimu.
No comments:
Post a Comment