
ARSENE WENGER, Bosi wa Arsenal,
akisikitishwa kukosa kunyakua Nafasi ya Kwanza ya Kundi lao la UCL, UEFA
CHAMPIONZ LIGI, sasa anaomba Mungu wabahatike kupata ‘ubwete’ katika Droo ya Raundi
ya Mtoano ya Timu 16 itakayofanyika Jumatatu Desemba 16.
Arsenal, ambao Jana walichapwa Bao 2-0
na Napoli na kutupwa Nafasi ya Pili huku Nafasi ya Kwanza ikichukuliwa na
Borussia Dortmund walioifunga Marseille 2-0 katika Mechi za Kundi F, wanaweza
kukutana na moja kati ya Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid, Paris
St-Germain au Atletico Madrid katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WA MAKUNDI
|
TIMU ZA PILI ZA
MAKUNDI
|
-Manchester United
-Real Madrid
-Paris St-Germain
-Bayern Munich
-Chelsea
-Borussia Dortmund
-Atletico Madrid
-Barcelona
|
-Bayer Leverkusen
-Galatasaray
-Olympiacos
-Manchester City
-Basel
-Arsenal
-Zenit St.
Petersburg
-AC Milan
|
***DROO: Mshindi
wa Kundi anapangiwa Timu za Pili za Makundi ila Timu za Nchi moja au toka Kundi
moja haziruhusiwi kukutana.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Wenger ametamka: “Kumaliza Nafasi ya Pili
kunafanya Droo yetu kuwa ngumu. Katika Miaka mine, mitano iliyopita tumekuwa na
Droo ngumu labda Mwaka huu!”
Msimu uliopita, kwenye Raundi ya Mtoano
ya Timu 16, Arsenal walipangiwa na Bayern Munich na kufungwa Bao 3-1 Uwanjani
Emirates na kushinda 2-0 huko Allianz Arena na Bayern kusonga Bao la Ugenini na
hatimae kutwaa Ubingwa.
WAKATI HUO HUO,
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anataka wapangiwe
Galatasaray, Timu anayochezea Staa wake wa zamani, Didier Drogba.
Drogba aliondoka Chelsea Juni 2012
baada ya kukaa huko kwa Miaka minane.
Mourinho amesema: “Galatasaray ni
wagumu lakini nataka Didier aje hapa na kuhisi ninachosikia.”
Chelsea, kwa kumaliza Washindi wa Kundi
E, wanaweza kupangiwa moja kati ya meet Bayer Leverkusen, Galatasaray, Zenit St
Petersburg, Olympiakos au AC Milan.
Hata hivyo, Mourinho amekiri yeyote
watakayopangiwa, Mechi itakuwa ngumu kwani kila Timu Ulaya ni ngangari.
UCL-Ratiba:
-Raundi ya Mtoano
Timu 16: 18/19/25/26 Feb na
Marudiano11/12/18/19 Machi
-Robo Fainali: 1/2 Aprili na Marudiano 8/9 Aprili
-Nusu Fainali: 22/23 Aprili na Marudiano 29/30 Aprili
-Fainali: 24 Mei
MATOKEO:Jumatano 11 Desemba 2013
Galatasaray 1 Juventus 0 [Mechii hii ilianza Jumanne na kumalizwa Jumatano]
FC Schalke 2 FC Basel 0
Chelsea FC 1 FC Steaua Bucureşti 0
Olympique de Marseille 1 Borussia Dortmund 2
SSC Napoli 2 Arsenal 0
FK Austria Wien 4 Football Club Zenit 1
Club Atlético de Madrid 2 FC Porto 0
AC Milan 0 AFC Ajax 0
FC Barcelona 6 Celtic 1
++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment