
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete hapo jana,
Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani
na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha
aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R
Mandela.
Maelfu kwa
maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye
Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa
ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika
Mashariki.
Mheshimiwa
Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa
Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto
we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.
Baada ya
kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza
wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia kipindi
kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.
Kiasi cha
viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na
kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine
wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla
ya saa tano.
![]() |
| Rais Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Marekani Georgr Bush |
Mbali na Rais
Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri
duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa Marekani,
Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa
David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu
hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu
wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na
Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza,
Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais Kikwete leo,
Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia katika kutoa
heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa
kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini
Pretoria.
![]() |
| Rais Kikwete na Mama Salma wakiwa Mzee Mandela enzi za Uhai wake |


No comments:
Post a Comment