FDL:
MECHI ILIYOVUNJIKA STAND, KANEMBWA KURUDIWA TABORA
Release No. 209
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Desemba 16, 2013
MECHI YA STAND,
KANEMBWA KURUDIWA TABORA
Mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa Novemba 2 mwaka huu Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga na kuvunjika, sasa itarudiwa Februari 1 mwakani.
Uamuzi huo umefanya na Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB) katika kikao chake kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam
ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia ripoti za mchezo huo uliovunika dakika
ya 87.
TPLB imefikia uamuzi huo baada ya
kujiridhisha kuwa mwamuzi Peter Mjaya alitoa taarifa ambazo si sahihi kuhusu
mechi hiyo. Mjaya ameondolewa kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
FDL.
Mechi hiyo itarudiwa katika Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo timu zote zimetumiwa uamuzi huo kwa
maandishi.
Vilevile wachezaji tisa wa Kanembwa JKT
waliompiga mwamuzi katika mechi hiyo suala lao linapelekwa Kamati ya Nidhamu ya
TFF kwa ajili ya hatua zaidi kwa mujibu wa Ibara ya 27(g)(3) ya Kanuni za FDL.
Wachezaji hao ni Abdallah Mgonja,
Baliki Abdul, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement, Mrisho Musa, Mtilakigwa Hussein,
Nteze Raymond, Philo Ndonde na Uhuru Mwambungu.
TANZANITE, BATSESANA
KURUDIANA DES 21
Mechi ya marudiano ya raundi ya pili
kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri
chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini (Batsesana)
itachezwa Jumamosi, Desemba 21 mwaka huu.
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa
Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za
Afrika Kusini. Tanzanite itaondoka Jumatano, Desemba 18 mwaka huu saa 4 asubuhi
kwa ndege ya Fastjet ikiwa na msafara wa watu 29 wakiongozwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TFF, Khalid Abdallah.
Kikosi hicho kitaagwa kesho (Desemba 17
mwaka huu) saa 6 katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura
Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment