
AVB ATIMULIWA
LEO Tottenham imemfukuza kazi Meneja
wao Andre Villas-Boas mara baada ya Jana kunyukwa Bao 5-0 na Liverpool.
Kipigo hicho cha Jana ndio kimekuwa
kisago kikubwa kwa Timu hiyo kwa Miaka 16 Uwanjani kwao White Hart Lane na
kimewaacha wakiwa Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 8 nyuma ya
Vinara Arsenal.

Villas-Boas, Miaka 36, aliteuliwa
Meneja Tottenham Julai 2012.
Mwezi Machi 2012, Villas-Boas
alifukuzwa kazi Chelsea baada ya kuwa hapo kwa Miezi minane tu.
Tottenham ilipigwa Bao 6-0 na Man City
hapo Novemba 24 na, ingawa walitoka Droo na Mabingwa Man United na kuzifunga
Fulham na Sunderland, kipigo hiki cha Liverpool kimewachukiza Wamiliki wa Klabu
hiyo ambayo mwanzoni mwa Msimu ilimuuza Gareth Bale kwa Dau la Pauni Milioni 85
kwa Real Madrid, ikiwa ni Rekodi ya Dunia, na kununua msululu wa Wachezaji
ambao ni Paulinho, Roberto Soldado, Nacer Chadli, Etienne Capoue, Christian
Eriksen, Vlad Chiriches na Erik Lamela lakini Timu imekuwa ikifanya vibaya
kwenye Ligi.
Hata hivyo, kwenye michuano ya Ulaya ya
EUROPA LIGI, Tottenham imekuwa ikifanya vyema na kushinda Mechi zao zote 6 za
Kundi lake na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ambako leo wamepangiwa
kucheza na Dnipro, Klabu ya Ukraine.
Mbali ya mafanikio hayo, Villas-Boas
pia ameipeleka Tottenham kwenye Robo Fainali ya Capital One Cup ambako Desemba
8 watacheza na West Ham.
Villas- Boas anakuwa Meneja wa 5 Msimu
huu kutimuliwa kazi toka Klabu ya Ligi Kuu England wengine wakiwa Steve Clarke,
aliefukuzwa Jana kutoka West Bromwich Albion, pamoja na Paolo Di Canio
aliefukuzwa Sunderland Mwezi Septemba, Ian Holloway alitimuliwa Crystal Palace
Mwezi Oktoba na Martin Jol aliepoteza kazi Fulham Wiki 2 zilizopita.
Wakati Huohuo
SERGIO AGUERO NJE
MWEZI!
Kwa mujibu wa Meneja wa Manchester City
Manuel Pellegrini Nyota wao Sergio Aguero atakuwa nje kwa Mwezi mzima akiuguza
Musuli za Mguu.

Aguero aliumia mapema Kipindi cha Pili
hapo Jumamosi wakati City inaichapa Arsenal Bao 6-3.
Miongoni mwa Mechi muhimu ambazo Aguero
atazikosa ni ile dhidi ya Liverpool lakini wapo wenzake, kina Alvaro Negredo,
Edin Dzeko na Stevan Jovetic, ambao wanaweza kuziba nafasi yake.
MECHI ZINAZOFUATA ZA
MAN CITY:
|
17 Desemba
|
Leicester v Man
City
|
LC
|
|
21 Desemba
|
Fulham v Man City
|
LKE
|
|
26 Desemba
|
Man City v
Liverpool
|
LKE
|
|
28 Desemba
|
Man City v Palace
|
LKE
|
|
1 Januari
|
Swansea v City
|
LKE
|
+++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment