HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 5 December 2013

"PATA TAARIFA ZA BARCLAYS PREMIER LEAGUE HAPA" MAN UNITED YAPIGWA, ARSENAL, CHELSEA, CITY, LIVERPOOL ZASHINDA!!



>>SHUJAA LUIS SUAREZ APIGA 4, AWEKA HISTORIA LIGI KUU ENGLAND!!
MABINGWA Manchester United wamefungwa Nyumbani kwao Bao 1-0 na Everton wakati Arsenal, Chelsea, Manchester City na Liverpool zote zikishinda Mechi zao za Ligi Kuu England Jana Usiku.

Hii ni mara ya kwanza kwa Everton kuifunga Man United Uwanjani Old Trafford tangu Mwaka 1992 na kipigo hicho kimewaacha Man United wawe Nafasi ya 9 Pointi 12 nyuma ya Vianara Arsenal.

Bao la ushindi la Everton lilifungwa na Bryan Oviedo katika Dakika ya 86 na kuipa Everton ushindi wa Bao 1-0 ikiwa ni Mechi ya kwanza kwa Meneja wa Man United David Moyes kuivaa Timu yake ya zamani Everton.
Vinara wa Ligi Arsenal waliichapa Hull Cuty Bao 2-0 kwa Bao za Nicklas Bendtner na Mesut Ozil na kuwaweka Pointi 4 juu kileleni mwa Ligi.

Katika Mechi za Jana, shujaa ni Luis Suarez aliepachika Bao 4 wakati Liverpool inaichapa Norwich City Bao 5-1 na kuweka Historia ya kuwa Mchezaji wa kwanza katika Ligi Kuu England kufunga Hetitriki 3 dhidi ya Klabu hiyo hiyo moja.
Katika Misimu miwili iliyopita, Suarez amekuwa akipiga Hetitriki Uwanjani Carrow Road Nyumabini kwa Norwich City.
Bao jingine la 5 la Liverpool lilifungwa na Raheem Sterling.
Huko Stadium of Light, ilikuwa piga nikupige kati ya Sunderland na Chelsea hadi Chelsea kuibuka Mshindi kwa Bao 4-3.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard (Dakika ya 36 na 62 minutes), Frank Lampard (17) na Bao la kujifungwa mwenyewe Phil Bardsley (84) huku Sunderland wakifunga toka kwa Jozy Altidore (14), John O'Shea (50) na Bardsley (86).
Manchester City nao walikuwa na mshikemshike na West Brom na hatimae kushinda Bao 3-2 na kujiweka Pointi 2 nyuma ya Chelsea na Pointi 1 mbele ya Liverpool na Everton.
Bao za Man City zilifungwa na Yaya Toure, Bao 2, na Sergio Aguero na kujikuta wakiongoza lakini WBA wakaja juu na kupiga Bao 2 kupitia Costel Pantilimon, aliejifunga mwenyewe na Victor Anichebe.

Bryan Oviedo akifunga dhidi ya Man U jana

MATOKEO:
Jumatano Desemba 4
Arsenal 2 Hull City 0
Liverpool 5 Norwich 1
Man United 0 Everton 1
Southampton 2 Aston Villa 3
Stoke 0 Cardiff 0
Sunderland 3 Chelsea 4
Swansea 3 Newcastle 0
Fulham 1 Tottenham 2
West Brom 2 Man City 3
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]

Jumamosi Desemba 7
1545 Man United v Newcastle
1800 Crystal Palace v Cardiff
1800 Liverpool v West Ham
1800 Southampton v Man City
1800 Stoke v Chelsea
1800 West Brom v Norwich
2030 Sunderland v Tottenham

Jumapili Desemba 8
1630 Fulham v Aston Villa
1900 Arsenal v Everton

Jumatatu Desemba 9
2300 Swansea v Hull

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
14
19
34
2
Chelsea
14
14
30
3
Man City
14
26
28
4
Liverpool
14
13
27
5
Everton
14
9
27
6
Tottenham
14
-2
24
7
Newcastle
14
-2
23
8
Southampton
14
5
22
9
Man Utd
14
4
22
10
Aston Villa
14
0
19
11
Swansea
14
1
18
12
Hull
14
-6
17
13
West Brom
14
-2
15
14
Stoke
14
-6
14
15
Cardiff
14
-9
14
16
Norwich
14
-16
14
17
West Ham
14
-3
13
18
Fulham
14
-14
10
19
Crystal Palace
14
-14
10
20
Sunderland
14
-17
8
 

No comments:

Post a Comment