Na Oscar Asenga Tanga
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema)kimesema kuwa licha ya kuwepo msuguano wa ndani lakini kimetamba kuwa
kitachukua kata zote sita zilizopo kanda ya kaskazini katika uchaguzi
utakaofanyika hivi karibuni hapa nchini.
Uchaguzi huo wa marudio unatokana na kata za Kiomoni,Mtae mkoani Tanga na Sombetini mkoani Arusha,Kiborolioni mkoani Kilimanjaro na Karachimbi Kiteto mkoani Manyara kutokuwa na madiwani wake kutokana na baadhi yao kujiuzulu na wengine kufariki dunia.
Tambo hizo zilitolewa na Katibu wa
Chadema Kanda ya Kaskazini,Amani Golugwa wakati akizungumza na viongozi wa
chama hicho mkoani hapa kwenye mafunzo ya Chadema ni msingi ambayo yalikuwa na
lengo la kuwajengea uwezo pamoja na kukabidhi vifaa vya awali vya kampeni kwa
kata zinazokabiliwa na uchaguzi huo ambazo ni Kiomoni na Mtae
Golugwa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa awamu ambapo awamu ya pili watakabidhi pikipiki ili viongozi wa chama hicho waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo na hatimaye kuweza kupata ushindi kwenye chaguzi hizo.
Alisema chama hicho kitaingia kwenye mchakato
huo kwa kuangalia wanachama ambao watakao kuwa na uwezo wa kuipeperusha bendera
yao kwa kuweka wagombea wanaokubalika kwa wananchi kwenye kata zao.
Katibu huyo alisema kuelekea kwenye
mchakato huo aliwataka wanachama kuwa na mshikamano wa dhata ambao utakiwezesha
chama hicho kupata ushindi na kuacha kutengeneza makundi yasiyo na tija.
|
Katibu wa chadema
kanda ya kaskazini,amani golugwa katikati akikabidhi vifaa kwa mwenyekiti wa
chadema kitongoji cha luande kata ya kiomoni mwanamtama bakari kushoto na
kulia ni katibu wa chadema mkoa wa tanga,jonathan bahweje.
|
“Tunataka kutengeneza
historia kwa madiwani wawili kwenye jimbo la Tanga na kata nyingine zilizopo
mikoa ya kanda ya kaskazini “Alisema Golugwa.
Akizungumzia mafunzo hayo,Golugwa
alisema mafunzo hayo ya siku mbili yana lengo la kuwajengea uwezo wanachama
wake mkoani Tanga pamoja na kukiimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi ujao.
Waliopokea vifaa hivyo ni Mwanamtama
Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema kitongoji cha Luande kata ya Kiomoni
Jimbo la Tanga na Edward Ngereza wa Kata ya Mtae Jimbo Mlalo wilayani Lushoto.
|
Wanachama wa chama
hicho mkoani tanga wakimsikiliza katibu wa kanda ya kaskazini,amani golugwa
ambaye hayupo pichani leo
|

No comments:
Post a Comment