![]() |
| Samatta akishangilia na Kiemba pamoja na Ulimwengu. |
TIMU
ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga hatua ya
robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati,
CECAFA baada ya kuitafuna Burundi bao 1-0 alasiri ya leo.
Shukurani
kubwa zimwendee nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya TP Mazembe, Mbwana
Samatta aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 7 akiunganisha kwa ufundi
mkubwa krosi iliyochongwa na Mtanzania mwenzake anayekipiga klabu ya Tp
Mazembe, Thomas Ulimwengu.
Stars
imecheza soka zuri na kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini umahiri wa kipa
wa Burundi, Arakaze Arthur amewaokoa Warundi kwani aliokoa bunduki nyingi
langoni mwake.
Kwa
Matokeo ya mchezo wa leo, Kili Stars imemaliza mechi za makundi ikijikusanyia
pointi 7 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia, kisha kuifunga Somalia 1-0
mechi za awali, na leo hii kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burundi.
Nani
atakuwa kinara wa kundi B, matokeo ya mchezo unaoendelea sasa baina ya Zambia
na Somalia utaamua ambapo mpaka sasa ni mapumziko na Zambia wako mbele kwa
mabao 2-0.
Kama
Zambia itaibuka na ushindi mkubwa leo hii basi itaongoza kundi B, na tafsiri
yake ni kuwa Kilimanjaro Stars itakumbana na Uganda katika mchezo wa robo
fainali.
Iwapo
Kili stars itakutana na Uganda, itakuwa na hamu ya kulipa kisasi kwani walilala
3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa michuano iliyopita mjini Kampala, Khamis
Kiiza na Emmanuel Okwi wakiwemo ndani kwani mwaka huu pia wamejumuishwa kwenye
kikosi cha Uganda The Cranes.
kama
Stars itaongoza Kundi B, itakutana na Timu ya Taifa ya Rwanda, `Amavubi` .
Tanzania
Bara; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank
Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Amri Kiemba/Haroun Chanongo dk77, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81.
Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.
Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.

No comments:
Post a Comment