
AFRIKA KUSINI KUTUA KWA SOUTH AFRICA AIRWAYS
Kikosi cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu). Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.
Wanaounda Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni na
Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani, Caryn van Reyneveld, Chamelle
Wiltshire, Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, Tiisetso Makhubela na Vuyo
Mkhabela.
Viungo wapo Amanda November, Amogelang Motau, Gabriella Salgado,
Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili
Makhoali, obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya. Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) ni sh. 1,000 kwa
viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa
VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

RAIS TFF AUNDA KAMATI MBILI MAALUMU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.
Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani
wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF,
Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim
Bawazir na Lucas Kisasa.
JOPO LA WATAALAMU KUPANGA MKAKATI WA AFCON 2015
Jopo la wataalamu 20 walioteuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi linakutana kupanga mkakati wa kuonesha jinsi Tanzania inavyoweza kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2015 nchini Morocco. Kikao hicho maalumu (retreat) kitafanyika mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6-8 mwaka huu.
Jopo hilo litaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Omari Kipingu. Wengine wanaounda jopo
hilo linalohusisha pia makocha ni Dk. Mshindo Msolla, Peter Mhina, Ayoub
Nyenzi, Abdallah Kibaden, Pelegrinius Rutahyuga, Kidao Wilfred, Salum Madadi,
Juma Mwambusi, Ken Mwaisabula, Boniface Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul
Mingange, Ally Mayay, Boniface Mkwasa na Dan Korosso.
Wajumbe wengine wa
jopo hilo wanatoka Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
No comments:
Post a Comment