Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela
amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza
Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya
kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela
alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini
kwa miezi mitatu.
Katika
taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela
amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo
mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kuwa mwanawe wa kume alifariki
kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais
Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela
aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais
aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka
gerezani.
Hakuonekana
sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004.
Tanzania
imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013,
kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais
Jakaya Kikwete wa pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera
zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia
kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa
Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote
na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela
kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
Rais
amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo
wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa
Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya
ubaguzi wa rangi.
Mandela
amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye
aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi
baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela
alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini
kwa miezi mitatu.

HISTORIA
YAKE
Rolihlahla
Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika
mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918.
Alikuwa
mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza
kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson.
Alitoroka
mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana
na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky
na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)
Mandela
alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na
mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa
huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi.
Akihofiwa
kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela
kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya.
Alikamatwa
mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada
ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958,
Mandela alimuoa Winnie Ma
Sheria
ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji 69 mjini
Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza kisasi na hivyo
kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha harakati zake za
kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.
Mwaka
1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama
wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma.
Yeye na wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964.
Huru hatimaye
1990
Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC.Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.
No comments:
Post a Comment