![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa |
Na
Oscar Assenga, Muheza.
MKUU wa Mkoa wa
Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amewataka madereva mkoani Tanga kuhakikisha
wanajiepusha na ajali barabarani kwa kutoendesha mwendo kasi hasa katika
kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
| Mkuu wa Mkoa akikabidhi Misaada hiyo |
Gallawa alitoa kauli
hiyo juzi wilayani hapa wakati akizungumza wananchi wa mkoa wa Tanga mara baada
ya makabidhiano ya zawadi za krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi ya wazee wasiojiweza
misufini kata ya Ngomeni wilayani hapa.
Alisema
kuwa mara nyingi wakati wa sikukuu na mwishoni mwa mwaka madereva wengi
wamekuwa wakiendesha magari yao kwa mwendo kasi bila kujali kuwa wanaweza
kukumbana na ajali na kupoteza maisha ya watu pamoja na kuleta simazi kwa
Taifa.
| Misaada iliyotolewa |
“Nasisitiza
madereva acheni kuendesha magari mwendo kasi kwani bado tuna majonzi ya ajali
zilizotokea ndani ya mwaka huu na kusababisha maisha ya raia wasio na hatia
kukatizwa huku wengine wakibaki na ulemavu wa kudumu “Alisema Gallawa.
Katika hatua
nyengine, Gallawa aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kudumisha utulivu na
amani kwa kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani na kuwa mstari wa mbele
kutoa taarifa kwa vyombo husika kwa viashiria vya kutoweka kwa amani.
Hata hivyo mkuu wa
mkoa huyo alisisitiza suala la usafi katika maeneo mbalimbali jijini hapa kwa
kuwataka wananchi kuendelea kuyaweka mazingira yao katika muonekano mzuri kwa
wageni na wenyeji.
Katika makadbidhiano
hayo, Mkuu huyi wa mkoa alikabidhi zawadi zilizotoka kwa Mh.Rais mchele Kilo
150, mbuzi watatu(3),na mafuta ya chakula lita 40,miche mitano ya sabuni pamoja
na katoni moja ya chumvi vyote vikiwa na thamani ya fedha taslimu sh.615,000.
Wakati huo huo,Jeshi
la Polisi Mkoa wa Tanga limesema hakuna matukio matukio makubwa yaliyojitokeza
katika kusheherekea sikukuu ya krismas iliyoazimishwa jana katika maeneo
mbalimbali nchini.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Constatine Massawe alisema
jeshi la polisi mkoani hapa limejipanga vizuri katika kukabiliana na
matukio yoyote ya kiuhalifu ambayo yanaweza kujitokeza katika kipindi hiki cha
sikukuu na mwisho wa mwaka.

No comments:
Post a Comment