HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 29 December 2013

TANGA YAINGIA HATARINI KUPOTEZA HADHI YA JIJI


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa

Halmashauri  ya Jiji la Tanga inaweza kushushwa hadhi kuwa manispaa kutokana na kushindwa kukusanya mapato.
Hayo yalibainishwa jana na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati wa majumuisho ya ziara yao.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajabu Mbaruk, alisema kamati inakwenda kuishauri serikali kushusha hadhi ya kuwa jiji na kurudi katika hadhi ya manispaa kwa kuwa imeshindwa kukusanya mapato.
 
Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Tanga inatia aibu kwani inakusanya mapato ya Sh. bilioni 3.5 kwa mwaka ambayo ni madogo kulinganisha na ya Jiji la Mwanza ambalo linakusanya Sh. bilioni 10 kwa mwaka.

Alisema cha kusangaza, Halmashauri ya Jiji la Tanga ina vyanzo vingi vya mapato, lakini mapato hayakusanywi na kusema kuwa hiyo ni aibu na haifai kuwa na hadhi ya jiji.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Juliana Malange
 

Mbarok alisema kuwa madiwani na watendaji hawana uchungu na halmashauri ya jiji la Tanga. “Sasa kamati inakwenda kuishauri serikali kushusha hadhi jiji la Tanga kuwa manispaa kama zamani,” alisema.
Alisema kuwa Mkoa wa Tanga una wilaya tisa, lakini cha kushangaza ni kuwa mkoa mzima wanakusanya Sh. bilioni nane tu na kuzidiwa na Jiji la Mwanza.
 
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kiasi cha Sh. bilioni mbili za mapato zimepotea kutokana na jiji hilo kutokuwa na uwezo wa kutunza vizuri kumbukumbu za mahesabu.

Alipoulizwa na wanahabari  kuhusiana na lini LAAC itakutana na serikali ili kuwasilisha pendekezo la kulishusha hadhi Jiji la Tanga, alisema  kamati yake inaandaa taarifa ya mapendekezo na ili kuipeleka  Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).
 

No comments:

Post a Comment