|
RC Iringa Dr
Christine Ishengoma
|
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma ametuma
salama kali za Krismas na Mwaka mpya kwa
wafanyabiashara watakaopandisha bei ya vyakula msimu
huu wa sikukuu kuwa watachukulia hatua kali.
Huku
akiwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya ,wakuu wa
wilaya ,maofisa biashara wa wilaya na mkoa huo
kuanza kuzunguka mitaani kuchunguza bei ya bidhaa
na kuwataka kuchukua hatua kwa wote wanaliopandisha bei
kiholela.
Akizungumza
na wanahabari jana ofisini kwake ,mkuu huyo wa
mkoa alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya
wafanyabiashara kutumia sikukuu mbali mbali kujipatia
fedha kwa kuwanyonya wananchi jambo ambalo katika mkoa huo halitavumiliwa
kamwe.
Alisema
kuwa lengo la serikali ya mkoa kuwabana
wafanyabiashara ni kutaka kuona wananchi wanasherekea
sikukuu hizo na kununua vyakula na vitu mbali
mbali vya sikukuu kulingana na bejeti waliyoitenga kwa
sikukuu hizo.
"
Serikali ya mkoa haitakubali kuona wananchi
wakiibiwa kwa kuuziwa vyakula kwa bei kubwa za
sikukuu....tumejipanga kuchukua hatua kali na tunaomba
wananchi pia kutoa ushirikiano "
Hata hivyo
mkuu huyo wa mkoa alivipongeza vyomba vya habari mkoani
Iringa kwa mchango mkubwa wa kuhamasisha maendeleo na
kutaka kuonyesha ushirikiano katika wakati huu wa sikukuu kwa kufanya
chunguzi wa wafanyabiashara wanaopandisha bei.
Katika hatu nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbali mbali yakiwemo yale yanayohimili ukame kwa maeneo yenye changamoto ya mvua.
Pia
aliwataka maofisi kilimo na mabwana shamba kuachana na
mpango wa kuvaa suti na kushinda maofisini wakati huu wa
msimu wa kilimo badala ya kwenda kuwaelimisha wakulima .
Dr
Ishengoma aliwataka wakulima kuendelea kutumia
mbolea ya Minjingu ambayo alidai hata yeye amekuwa
akiitumia na ni miongoni mwa mbolea bora nchini na kuwataka kuepuka
maneno ya kukatisha tamaa yanayoendelea kutolewa na watu juu ya
mbolea hiyo.
Wakati huo
huo serikali ya mkoa wa Iringa imepiga marufuku
wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda kushiriki madisco toto
ambayo alidai ni hatari na ni vema wazazi na walezi wa watoto
mkoani Iringa kuwa makini na kuachana na tabia ya kuwaacha
watoto wao peke yao wakati huu wa sikukuu.
No comments:
Post a Comment