
Na
Oscar Assenga,Tanga.
BONDIA Haji Juma wa
Tanga anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Mohamed Mzungu wa Zanzibar
katika pambano la kuwania Ubingwa wa Tanzania (TPBO) kg 52 superfly la raundi
10 litakaofanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Tangamano jijini Tanga.
Mratibu wa Pambano
hilo, Promota Ally Mwazoa alisema pambano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake
kutokana maandalizi yaliyofanywa na uwezo walionao mabondia hao.
Mwazoa aliyataja
mapambano ya utangulizi kuwa ni bondia Rajabu Mahoja na Jumanne Mohamed wote
kutoka mkoani Tanga wataonyeshana kazi pambano la raundi 10 lenye uzito wa kg
57 feith weight.
Licha ya kuwepo
pambano hilo mabondia wengine watakaozichapa ni Hamisi Mwakinyo wa Tanga
atapambana na Said Mundi litakalokuwa la uzito wa kg 59 super feather raundi 6
huku Saimon Zabron naye atapigana na Athumani Boxers pambalo litakalo kuwa na
uzito wa kg 61 Light weight raundi sita.
Mratibu huyo alisema
pambalo lengine litakalo hitimisha raundi sita ni bondia J.J Ngotiko wa Tanga
ambaye atapanda ulingoni kuzichapa na Zuberi Kitandula litakalokuwa la raundi
sita super bantam.
Aliyataja mapambano
ya mwisho siku hiyo yatakuwa na raundi nne nne ambapo bondia Jacob Maganga
atazichapa na Mohamed Kidari pambano lenye uzito wa kg 65 light walter raundi
nne wakati Juma Mustapha atapambana na Selemani Hamza litakalokuwa la raundi
nne lenye uzito wa kg 55 super bantam.
Mratibu huyo alisema
siku ya mapambano hayo,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa msanii nguli wa filamu hapa
nchini King Majuto.
No comments:
Post a Comment