Na Thehabari.com, Namanyere-Nkasi
MWALIMU mmoja
wa Shule ya Msingi Sintali (jina tunalo) anatuhumiwa kwa kuwatia mimba
wanafunzi wawili mmoja akiwa wa shule anayofundisha yeye na mwingine wa Shule
ya Sekondari Sintali hali iliowafanya wanafunzi hao kukatisha masomo.
Tukio hilo
limetokea Katika Kijiji cha Sintali, Wilaya ya Nkasi na baada ya taarifa kuenea
kijijini hapo mwalimu huyo alitoroka kituo chake cha kazi na kukimbilia pasipo
julikana. Akizungumzia tukio hilo Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw.
Misana Kwangura alisema mwalimu huyo anadaiwa kufanya kosa hilo tangu mwezi
Agosti, 2013 na baada ya kuanza kufuatiliwa alikimbia kituo chake cha kazi.
Alisema baada
ya kutoroka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ulilazimika kusitisha
mshahara wake jambo ambalo lilimlazimu ajilete mwenyewe ndipo alipokamatwa na
kufunguliwa mashtaka kwa kosa linalomkabili.
Hata hivyo
Kwangura alisema wanafunzi hao mmoja wa darasa la saba na mwingine wa kidato
cha pili wamekana mwalimu huyo kuwatia mimba na kudai wametiwa mimba na watu
wasiojulikana ambao walikuja kijijini hapo kununua mazao. Mwalimu huyo amekana
kuhusika na kitendo hicho.
Pamoja na
hayo Jeshi la Polisi limemuachia mwalimu huyo baada ya kukosa ushahidi wa
kumtia hatiani.
“…Uongozi wa
Kijiji pamoja na wa shule wanaamini kuwa yeye (mwalimu huyo) ndiye aliyewatia
mimba lakini wao wanakataa, sisi tunaamini wanamtetea ili asichukuliwe hatua za
kisheria lakini sisi hatujakubali tunasubiri wanafunzi hao wajifungue kasha
tutatumia DNA kupima tujue ukweli…tayari mmoja amejifungua tunamsubiri
mwingine,” alisema Ofisa Elimu, Kwangura.
Alisema
vipimo vitapelekwa kwa Mkemia wa Serikali ili hatuhakikishie bila utata.
Alisema tayari wamemkamata mwalimu mwingine wa Shule ya Msingi Itindi ambaye
naye amemtia mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa shule anayofundisha tangu
mwezi wa nane mwaka huu.
Huyu naye
baada ya kumtia mimba alipotea lakini baada ya kusitisha mshahara amejileta
mwenyewe na tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi Nkasi kwa kosa alilolifanya.
tuajabu huyo alikutoroka. Akizungumzia kwa ujumla matukio ya wanafunzi wa
Shule ya Msingi kutiwa ujauzito, Ofisa Elimu huyo alisema matukio ya mimba kwa
wanafunzi shule za msingi yanapungua kwa sasa kwani tangu Januari hadi Novemba
2013 jumla ya wanafunzi 9 wametiwa ujauzito na kukatizwa masomo yao, idadi
ambayo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo wanafunzi 11 walitiwa mimba.
Aidha
aliongeza kuwa kwa mwaka 2011 jumla ya wanafunzi 16 wa shule za msingi walitiwa
mimba na kukatizwa masomo yao. “…Kimsingi naweza kusema matukio haya kwa sasa
yanapungua ukilinganisha na hapo nyuma, na hii inatokana na elimu ambayo
tunaitoa kwa kuzunguka kwenye shule mbalimbali kwa kutumia ofisi ya Ofisa Elimu
Sayansi Kimu,” alisema Kwangura.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
kwa kushirikiana na TWMWA
No comments:
Post a Comment