HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 23 December 2013

GESI ASILIA NA MAFUTA VYAGUNDULIKA MKOANI TANGA "Ni huko Marungu na Tongoni"Mkuu wa Wilaya alonga"


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa

Serikali mkoani Tanga, imesema tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa kuwashirikisha watafiti wa kimataifa zimebaini kuwapo kwa mafuta na gesi asilia kwenye vijiji mbalimbali vilivyopo katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.

Nishati hizo zimebainika kuwapo katika wilaya za Tanga, Pangani na Mkinga na kwamba serikali kwa kushirikiana na watafiti hao wanaendelea na mchakato kufahamu kiasi kilichopo tayari kuanza kufanya majaribio ya rasilimali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendegu


Akizungumza katika mahojiano na wanahabari muda mfupi baada ya kufungua warsha ya wanahabari pamoja na asasi za kiraia kuhusu uzuruaji wa mafuta na gesi asilia iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Hifadhi Mazingira (WWF), Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu, alisema hatua hiyo ni mojawapo ya fursa za kiuchumi mkoani humu.

Dendego aliyataja maeneo ambayo hivi sasa yanafanyiwa utafiti na wataalam wa kimataifa kwa kutumia meli katika ukanda wa Bahari ya Hindi kuwa ni vijiji vya Marungu na Tongoni kwa upande wa Jiji la Tanga.

Akizungumzia hatua hiyo, Meneja Uhifadhi wa WWF, Gerad Kamwenda, alisema lengo hasa la kuwahusisha wanahabari katika mafunzo hayo ni kutokana na kutokuwa na usahihi wa habari zinazoandikwa kuhusu kuwapo kwa gesi na mafuta kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba nyingi hazifanyiwi utafiti wa kina. 

No comments:

Post a Comment