![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa Katabaro na kulia Afisa Habari Baraka Kiziuguto |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na waandishi wa
habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa Katabaro na kulia Afisa
Habari Baraka Kiziuguto
Uongozi wa klabu ya
Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha
mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba
22 mwaka huu.
Maamuzi hayo
yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu,
kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young
Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya
sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo
mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa
mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye
mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho
kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC
imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea
kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa
taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi
ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
Ikiwa Brandts
ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku
asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
Ili kuhakikisha timu
inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya
kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu
zote zitakapokamilika tutawajulisha.
Aidha uongozi upo
katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa
ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
Mwisho tunawaomba
wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya
bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika
kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati
ya Mashindano
Young Africans Sports
Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

No comments:
Post a Comment