HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 4 December 2013

HIVI NDIVYO KOCHA MPYA SIMBA ANAVYOANZA KAZI "HAKUNA KUREMBA"


Logarusic akiwa na Kikosi cha Msimbazi Mazoezini

KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ataweka sheria kali zitakazowabana wachezaji wake juu ya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Logarusic raia wa Croatia ambaye Jumatatu alisaini mkataba wa miezi sita kuifundisha Simba, alisema kuwa hakuna soka la ushindi bila ya nidhamu na anajua tabia za wachezaji wa Kiafrika ndiyo maana ameamua kuwatungia wachezaji kanuni hizo.

Kocha huyo alisema hazitakuwa kanuni kali ambazo zitaogopesha wachezaji lakini ni moja ya taratibu zake za kufundisha katika klabu yoyote anayofanyia kazi.

“Najua tabia za wachezaji duniani kote, lakini kwa Afrika nina uzoefu zaidi muda wowote unapotaka mafanikio katika timu lazima nidhamu iwe ya hali ya juu, bila ya hivyo hakuna utakalofanya.

“Kabla ya kuanza mazoezi nitawapa wachezaji sheria ambazo hawapaswi kuzivunja ili kuifanya timu iwe na nidhamu na kuwa mfano katika ligi, sheria hizi zitawafanya wawe makini ndani na nje ya uwanja,” alisema Logarusic mwenye umri wa miaka 51.
Alisema unapoendesha timu kwa misingi ya sheria ambayo kila mchezaji na mtendaji mwingine wa klabu ataifuata inakuwa rahisi kutimiza malengo ya kufanya vizuri uwanjani na hata kutwaa ubingwa.
Msimu huu aliyekuwa Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni mara kadhaa alikuwa akilalamika kuhusu utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wachezaji wake na aliwahi kutofautiana na kiungo wake Henry Joseph.

Katika hatua nyingine Logarusic alisema hamjui mchezaji yeyote wa timu hiyo, hivyo kila mchezaji anapaswa kujituma ili acheze kikosi cha kwanza.
Alisisitiza kuwa hawezi kutumia kikosi cha kwanza cha kocha aliyepita, yeye anaanza upya kupanga kikosi chake.
Hiyo huenda ikawa dalili njema kwa wachezaji wa timu hiyo ambao walikuwa hawapangwi mara kwa mara na kocha aliyetimuliwa Abdallah ‘King’ Kibaden.
 Baadhi ya wachezaji waliokuwa na wakati mbaya kwenye utawala wa Kibadeni ni Ramadhan Chombo’Redondo’, Amri Kiemba na Edward Christopher.
Logarusic amesema kuwa wachezaji wote wa Simba wana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na ataanza rasmi kazi ya kutafuta kikosi cha kwanza katika mazoezi yaliyotarajiwa kuanza jana jioni kwenye Uwanja wa Kinesi.

No comments:

Post a Comment